MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAUPONGEZA MGODI WA BUZWAGI.
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.





Wataalamu wa halmashauri ya mji wa Kahama wakiwa katika kituo cha kupozea umeme, kituo ambacho kinaelezwa kuwa kitatumika pia kufunga kifaa maalumu kilichonunuliwa na Mgodi wa Buzwagi ambacho kitawawezesha wananchi wa Kahama na viunga vyake kuweza kupata umeme wa uhakika.




Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.
Madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa namna ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.
Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya siku moja iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchimbaji.
“Kwa niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna ambavyo mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika kwa sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo mbinu mlioiweka katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za kisasa ” alisema Shija.
Mwenyekiti huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha upatikanaji wa kifaa kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa uhakika ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa Kahama kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi wa mji wa huo.
Akijibu ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na kukifunga.
“Kifaa kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu kuja na kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa uhakika.” Alisema Mwaipopo.
Ziara hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo, walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za mazingira na uchimbaji na kulifanya eneo hilo kuwa salama zaidi.
Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza ufahamu kwa Jamii kwa kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa kawaida kwa lengo la kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali ambayo wamesema itasaidia kupunguza taarifa za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani kutokana na Jamii kutokujua ukweli.
Post a Comment