KIJANA AWAFUNGIA NDUGU ZAKE NDANI NA KISHA KUCHOMA MOTO NYUMBA JIJINI MWANZA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nyumba moja iliyopo mtaa wa Kiseke Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza imeteketea kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo wakinusurika. 
Taarifa zinaarifu kuwa,  nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto 
Imeelezwa kuwa,  kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza kutokana na matatizo yake ya akili
Baada ya kumwaga mafuta  na kuwasha moto,  kijana huyo alitoweka na kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi kuwaokoa


Post a Comment
Powered by Blogger.