IDARA YA UHAMIAJI JIJINI DAR,YAWAHAMISHA MAOFISA WAKE 59

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Simu:  +255-22-2112035/40
          S.L.P.  9223
Nukushi:  +255-2122617/2120486
Barua pepe:ps@moha.go.tz
       Dar es Salaam


  

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imewahamisha jumla ya Maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji hamsini na tisa (59) kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake walikokuwa wakifanya kazi na kupelekwa sehemu mbalimbali nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema uhamisho huo umefanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Idara ya Uhamiaji. 

Kwa mujibu wa Jenerali Rwegasira zoezi hilo la kuwahamisha Maofisa wa Idara ya Uhamiaji linaendelea kufanyika nchi nzima ikiwa ni hatua za kuboresha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa kiutendaji.

Jenerali Rwegasira ameeleza kuwa watumishi wote waliopewa uhamisho wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vipya mara moja na kutoa angalizo kuwa mtumishi yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa visingizio mbalimbali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

5 Juni, 2016 

Post a Comment
Powered by Blogger.