MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» »Unlabelled » DRFA NA KIFA WAITWA TFF


Pamoja Blog 6/17/2016 10:26:00 PM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Kinondoni (KIFA) uliofanyika Juni 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.Kutokana na malalamiko hayo, TFF imewaita wagombea wote wa ngazi ya juu wa KIFA wakiwamo viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho kitakachofanyika kesho Jumamosi Juni 18, 2016 saa 3.00 asubuhi.Pia, imewaita viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sambamba na Kamati za Uchaguzi za DRFA kadhalika ile ya KIFA ambazo zilisimamia uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa mara ya pili mwishoni mwa wiki baada ya ule wa kwanza kuahirishwa mwezi uliopita.IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments