TUZO ZA WANAFUNZI BORA AFRIKA MASHARIKI "ALL-STARS STUDENTS AWARDS"ZAANZISHWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Aaron Ally(Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.
Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwl. Dany Mtanga) wameanzisha   Tuzo walizoziita All-stars Students Awards. 
Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari A-level na O-level za Afrika Mashariki.

Alhamisi hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.

Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye hayo masomo.
Tuzo hizo zitaaangalia  namba moja wote waliongoza katika nchi zote za Africa Mashariki
Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa sita.pia Special Talents, Michezo na  Shule bora
Post a Comment
Powered by Blogger.