PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA HAMSINI NA TISA (59)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


KUNA WATU WANACOPY HII STORY NA KUUZA KUAZIA KESHO UTARATIBU UNABADIRIKA WA KUISOMA HII STORY
Ukiitaji mwendelezo nitafute kwenye namba hii 0713363965 au kwenye hii blog ya www.pamoja.co.tz na sio sehemu nyingine.

Endelea.....................
Safari ya kuelekea mpaka wa Kenya na Somalia ilianzia kwenye nyumba ya yule Msomali rafiki yake na Shemeji Kitu kilichokuwa kikiisumbua akili yangu ni kutokujua ni jinsi gani shemeji ameweza kuwa na mtandao mkubwa kiasi kile mpaka nje ya nchi Mpaka hapo nikaamini shemeji ni zaidi ya Mafia na nikajua siwezi kupambana naye kirahisi namna hiyo kwa kumkimbia bali nitafute mbinu zaidi ya kupambana naye 
" Ila huyu shemeji ana weack point moja na ni mimi,ananipenda sana na najua hawezi kunfanya kitu kibaya hivyo yapaswa nitumie udhaifu huo kummaliza kabla hajanimaliza" niliendelea kuwaza Kwa muda huo woote Joan yeye kazi yake ilikuwa kulia peke yake,alilalamika sana huku lawama akinitupia mimi peke yangu 
"Usingenishawishi haya yote yasingenikuta Jun,nilikuwa naheshimiana na dada yangu ila ukanishawishi mpaka yamefika hapa" alilalamika sana " Baby naomba usimamishe gari kisssha unipe faragha ya kuongea na wewe maneno ya mwisho" nikajitutumua na kusema " Unahisi yatasaidia?" akauliza " Shida yangu sio hayo maneno yasaidie bali kuna kitu ambacho hukijui katika maisha yangu nahitaji ukijue kabla sijafa" nikasema Hapo nilikuwa najalibu kucheza karata ya mwisho kabisa katika tukio lile ili kuokoa nafsi yangu na ile ya Joan" 

Kipi sikijui kuhusu wewe? Labda kama una UKIMWI hapo naweza sema sijui hilo" akajibu " Usijal ila ni muhimu sana kuongea na wewe sasa hivi" nikasema " Kwa hiyo unatakaje? Si uongee hapa?" akasema " Sitaki mtu yeyote asikie maneno yangu kwa sababu yananihusu mimi na wewe peke yetu" nikasema " Ustaadhi tafadhali simamisha gari nimsikilize huyu" akamwambia yule Msomali " Utakuwa unacheza karata mbaya sana bana, kumbuka huyu kakufanyia jambo baya sana ukicheka naye atakujeruhi kabla yako" akasema yule Msomali Maneno ya yule msomali yalikuwa ya kweli na niliona wazi yanaweza yakazuia mbinu yangu kufanya kazi "
Shekhe najua naenda kufa,na wala siendi kumbembeleza huyu aahirishe madhumuni yake bali nahitaji kumwambia jambo la siri sana kuhusiana na siri zetu mimi na yeye ambazo hakuna anayezijua na kumbuka nikifa bila kumwambia hili jambo likitokea litamgharimu sana" nikasema Maneno yangu yakawaingia wote wawili nikawaona wakiinama kwa muda kila mmoja akimuwazia mwenzake na baadae gari zikasimamishwa Nikamfinya Joan kwa ishara ili aelewe kuwa pale najalibu karata ya mwisho ya kujiokoa " Haya ongea" akasema Shemeji "Siwezi kuongea hapa mbele za watu nitakuhalibia mambo yako yote hivyo naomba faragha na wewe" nikasema Shemeji aliniangalia kwa makini kwa muda kisha akawaomba wale watu watupe gari moja tusogee nayo kwa mabi kidogo " Lakini huogopi kuwa anaweza kukudhuru na kutukimbia?" akauliza yule Msomali " 
Hawezi hata kidogo,nafikili unanifahamu Ushtadhi sishindiw jambo,kumbuka ila kazi tuliyofanya Eldoret nilivyowalambisha mchanga wale askari jeshi wanne sembuse huyu kikaragosi asiye na mafinzo yoyote?" akajitapa shemeji " Sawa nakumbuka ila kumbuka huyu mtu yupo katika dakika za mwisho za kupigania uhai wake,anaweza kufanya chochote,kuwa zaidi ya makini" akasema Msomali " Usijali kwa hilo" akajibu Shemeji Tukapewa Range moja na shemeji akanilazimsha niendeshe mimi ili iwe ngumu kule ta ujanja ujanja Nikaendesha ile gari kwa kama mita mia tatu " Simamisha hapa kwa sababu umabu huu unatosha" akasema Nikasimamisha ile gari na kumgeukia kisha nikamtazama machoni kwa muda " Unaweza kuniambia?" akasema

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.