PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA HAMSINI NA NANE (58)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka kuona Joan analegea taratibu mpaka akaniangukia na kupoteza fahamu " Joan.....Joan......jaman huyu atakufa"nikasema kwa hamaki Hakuna aliyeoneshwa kushtushwa na hali ile ya Joan hivyonilibaki nikipambana mwenyewe " Tafadhal shem,mimi ndiye niliyekukosea na si Joan msaidie tumpeleke Hospitalini" nikaomba " Sinakutosha kweli Jun?" akauliza " Tuyaache hayo shem,tafadhali nakuomba msaidie" nikaendelea kubembeleza " 
Naona umejimilikisha,sasa unavyoniita shem ina maana Joan ndo mmiliki halafu mimi ndiye shemeji yako si ndiyo?" akauliza " Nisamehe baby msaidie" nikabadili usemi Hakuna aliyenijibu,safari iliendelea kwenda nje kidogo ya mji wa Mombasa Baada ya kutembea umbali kama wa kilometa sita gari ikaacha njia kuu na kuingia kwenye nyumba inayoelekea kwenye makazi ya watu.Gari ilienda mpaka kwenye jumba moja la ghorofa mbili zuri sana na geti jekundu likafunguliwa na tukaingia Baada ya gari kuingia na kusimama,tulishuka na Joan akabebwa na yale mabaunsa na kutolewa nje Kwa pale nje alitokea jamaa mwenye asili ya kisomali akiwa analindwa na vijawa wanne " Asalaam aleykum ustaadh" akasema shemeji " Aleykum salaam Ustadhat" akajibu Na wakakumbatiana kwa kupigana taratibu makofi mgongoni.
Kisha yule jamaa msomali akaja na kuniangalia " Vip huyu mbona kafa?" akauliza akimaanisha Joan " Hajafa sema anajifanya tu ili asikutane na adhabu" akajibu shemeji " Leteni maji tumwamshe" akatoa amri yule msomali Vijana wawili wakaondoka eneo lile na baada ya muda mfupi wakarudi na ndoo ya maji kisha wakamwagia Joan yote mwilini Haikuchukua muda Joan akashtuka na kuanza kukohoa kwa fujo kutokana na maji yale kuingia kwenye pua zake " Sasa ustadhi nashukuru kwa msaada wako kwanza"akasema shemeji " 
Wala usijal kwa hilo,kwani wewe ni sawa na ndugu yangu kwa sasa,bila wewe vijana wangu wangeshindwa kupenya siku ile uwanja wa ndege kule kwenu bana" akajibu " Ila bado nina ombi dogo" akasema shemeji " Ombi lako kwangu ni amri,sema na nitatekeleza" akajibu yule Msomali " Nahitaji kuwapa adhabu hawa vijana ambayo itawafanya wasinisahau milele aidha wakiwa hapa Duniani,au wakiwa huko akhera" akasema shemeji " 
Nafaham ila mimi nakushauri twende nao kwenye msitu wa Nyeri au kule Ukikuyuni na kuwapiga risasi kisha tuwatupe huko" akasema Msomali " Hiyo haitawatosha" akajibu Shemeji " Shehe mwenzangu Majid hapo nyuma anafuga Chui aliowashika huko Tanzania,unaonaje tukiwarusha pale ndani wawe chakula cha wale Chui?" akauliza tena Muda huo wao wanajadiliana nikiri wazi kuwa haja ndogo zilipenya taratibu sana kwenye suruali yangu na kuchuruzika kwenda chini " Eee! Mungu wangu,najua nimeshakukosea sana hapa Duniani ila na uhakika sijawa wa kufa,naomba sana uwepo wako uingie hapa na uweze kuninasua kwenye hili janga!
Nakuomba sana baba" nilikuwa nawaza " Baba nakuahidi ukinisaidia mara moja hii pekee nikipona hapa nitaokoka kabisa na kuwa mlokole,na kuacha dhambi zote,nisaidie baba mungu" Kumbe Joan naye alikuwa akiwaza yake " Baby ujue sisi ni binadam na hatujakamilika hivyo kukosea ni sehemu ya maisha yetu,naomba utusamehe na tunakuahidi kweli hatutarudia tena" nikasema huku machozi yakinitoka " Kweli dada hata sisi tuna mapungufu kama wanadamu wengine,ni tamaa ndo zimeniponza,tafadhali naomba unisamehe dadangu sitarudia" akasema Joan " Nyamaza!!!!" alifoka na kila mtu akakaa kimya "
Hata hilo la chui bado hawatapa maumivu nayotaka wayapate ustadhi,nipe wazo jingine,nataka wapate maumivu kidogo kidogo mpaka wajue wamekosa na wengine wajif*nze kupitia wao" akasema Shemeji " Sasa ngoja nikushauri kitu,tuondoke nao kwenda kwenye pori moja liko mpakani mwa Kenya na Somalia huko tutajua cha kufanya" akasema jamaa " Sawa,na nyie mbwa amkeni twende kwenye kifo chenu" alisema akimpiga Joan ngumi kali sana ya pua mpaka damu zikaanza kumtoka..

ITAENDELEA JUMAPILI
Post a Comment
Powered by Blogger.