PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA HAMSINI NA SABA (57)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka kiwango cha kuweza kuzimia ila nikabaki kujikaza ili nisije kuonekana nimeogopa mbele yake Ila kwa wakati huo mapigo yangu ya moyo yalikuwa kasi ambayo siwezi kuisema kabisa nilhisi kama moyo unataka kuchomoka Sijui kwa upande wa Joan ilikuwaje ila nilimuona akiinama chini " Mimi au sisi? Kwa sababu nipo peke yangu hapa" sijui akili hiyo niliipata wapi " Lakini nawaona mpo wawili?" akauliza " Huyu ni abiria mwenzangu na tumekutana tu kwa sababu ya safari na si zaidi" nikajibu " 
Sikia nikwambie Jun,wewe ni mtoto mdogo sana kwangu na ukweli ni kuwa huwezi kufurukuta japo kwa sekunde chache kama unataka kuendelea kuishi tulia usilete ujanja ujanja" akasema " Na mimi naomba nikwambie kitu,sikuogopi hata kidogo! Sawa? Sikuogopi kabisa na hapa nipo na mwanamke ninayempenda naomba utuache huru" nikaongea tena kwa ujasiri " Waoooh! Na wewe Joan unaamin hivyo? Unajidanganya! Jun kakuona siku moja kesho yake mkafanya mapenzi halafu anakudanganya anakupenda? Jun ni wa kwangu peke yangu na si mtu mwingine!" akafoka " 
Nampenda Joan tena sana na wewe sikupendi tuachie huru wetu tafadhali" nikasema Nilijalibu kuonesha ujasiri mbele ya shemeji ili nipate hadhi ya uanaume mbele ya Joan ila katika ukweli halisi nilikuwa namuogopa kuliko mwanajeshi " Sawa kama umesema hivyo ila nikuulize unahisi unaweza kunikimbia?" akauliza " 

Najua umenifunga kifaa chenye Gps na hicho kinasababisha kila nachokifanya ukione! Ila nakuahidi nitakiondoa tu siku moja na nitaishi huru" nikajibu " Hata ukikiondoa bado nina vijana wangu kila sehemu Jun hivyo huwezi nikimbia" akasema " Tambua kuwa siku moja nitakuwa huru kutoka mikononi mwako" nikasema " Sikia Jun,kuna kesi ya mauaji ya kaka yako ambayo nina uwezo wa kuifufua na kuigeuza kuwa ya kwako na ukumbuke wewe ndiye uliyemuua kweli na pia kuna kesi ya Dokta pia! Mtetezi wako ni mimi,kumbuka nafanya hivi kwa sababu nakupenda tena sana lakin naweza kukupoteza kwa sekunde chache sana" akafoka " 
Nilishaapa kuwa wewe ndiye mwanaume niliyewahi kumpenda peke yake hivyo atakayekatisha katikati yetu itabidi nimpoteze,sasa kama kweli unampenda Joan mwache aende huru na turudi nyumbani" akassema kwa upole " Nakufahamu Lily,hata nikimwacha hapa utatuma vijana wamuue,siko taayali bora utuue wote" nikajibu " Naona una kiburi sana eee? Sasa subiri uone mziki wangu" akajibu Kwa hasira shemeji aliondoka eneo lile na kwenda kukaa kwenye siti yake kisha akatulia " 
Sikia Joan tukifika uwanja wa ndege naomba twende kituo chochote cha polisi pale nje na kuripoti juu ya kutishiwa kuuawa na huyu mbwa ili tupate nafasi ya kumtoloka" Nikamwambia Joan " Sawa mpenzi ila jitahidi utoe hicho kifaa kinachosababisha atuone,yaan mimi hapa nahisi kifo kinaniita kabisa" akasema " Usijal baby nipo na wewe hawezi kukufanya kitu huyu" nikampa moyo Ila kwenye nafsi yangu nilimfahamu shemeji vizur sana na nilijua mziki wake hivyo nilitegemea chochote kile kutokea Tulifika uwanja wa ndege wa Mombasa kwa amani na kuanza kushuka Nilifatilia nyendo za shemeji pale wkati wa kushuka ila hakuonesha kuwa na haraka.
 Tulitumia ile nafasi ya shemeji kuzembea kutoka na kutoka haraka na Joan kisha tukachukua mizigo yetu na Joan tukaelekea eneo la ukaguzi Baada ya kukaguliwa tuliondoka eneo lile kwa kasi kwenda nje Huko nje tukaanza kuangaza angaza macho ili kutafuta kituo chochote cha polisi Tukabahatika kumuona askari mmoja tukamfata na kumwomba atuelekeze kitu Akatuchukua na kutupeleka kwenye gari moja nyeusi " Ingia hapa mtapelekwa kituo kilipo" akajibu Tuliingia kwenye ile gari ikiwa na dereva pekee akatuambia tunasubir askari yule ili tuondoke Ghafla kwenye lile gari akaingia shemeji na vijana watatu wenye mili mikubwa ya kimazoezi " Nafikiri wakati niliowaahidi wa mtu kulamba ardhi umefika kwa sababu mmshindwa kunisikiliza! Dereva twende" akasema Joan alianguka na kupoteza fahamu!!!

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.