PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA HAMSINI NA SITA (56)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Baada ya kupokea ile sms kutoka kwa shemeji nilijikuta nikitokwa na kijasho chembamba bila kutarajia Nikajibweteka kwenye kitanda cha pale Lodge kama mzoga! Nilichoka " Heeee! Mbona umebadilika ghafla baby? Kuna nini?"akauliza Joan Joan alipoona simjibu chochote aliichukua ile simu na kisha kuisoma ile sms Alichoka,na dhahiri akaoneka kuishiwa nguvu na yeye akaja na kujitupa kitandani 
Tulitulia kwa zaidi ya dakika kumi kila mmoja akiwaza ya kwake " Nahisi kuna mchezo unaucheza na huyo mke,nahisi mnataka kunitoa kafara" akasema Joan " Kafara? Kivip? Mbona sikwelew?" nikauliza kwa mshangao " Kama sivyo kwa nini kila tunachokifanya shemeji anajua? Na cha ajabu mpaka hotel hii kaifaham? Bora angefaham tuko huku pekee lakin mpaka hotel? Na amesema yuko hapa" akalalamika " Sikia baby,mimi na uhakika shemeji hayupo hapa Zanzibar ila kuna watu watakuwa wanatufatilia ili kumpa yeye taarifa" nikajibu " 
Hata kama lakini sio kwa mpaka hotel" akasema " Tuache kulaumiana ila cha msingi tutafute namna ya kufanya" nikajibu " Cha kwanza nenda kaangalie kama kweli yupo kisha njoo tubadilishe hotel" akashaur Joan Uzuri wa Joan ni kwenye ushaur,likitokea tatizo mimi wakati sijapata cha kufanya yeye huwa ameshapata jibu
 Nikatumia wazo la Joan na kuelekea sehemu ya chakula na kuangaza macho kila mahali sikumuona Nikazunguka sehemu mbalimbali za lodge ile ila sikumuona na hapo ikabidi nianze kuuliza baadhi ya wafanyakazi wa ile Lodge ila kila mmoja alidai hajaona mtu wa hivyo Nilipohakikisha sijaona chochote ikabidi nirudi chumbani " 

Kama nilivyokwambia, huyu atakuwa kaweka mtu kunifatilia cha msingi tuondoke hapa ila lazima tuwe makin" nikasema Joan hakuwa na kipingamizi,alibeba mizigo ambayo tulikuwa hatujaifungua na kuondoka eneo lile Nje tulipanda gari ya kukodi na kumwomba atutafutie Hotel nzuri tupumzike " Kaka hakikisha unapoendesha uwe unaafatilia kila gari inayoonekana nyuma yako,tunahisi kuna mtu anatufatilia" nilimweleza dereva.
 Kweli wakati tunaendelea na safari tukashtukia gari ikitufatilia ila kwa mbinu za yule dereva kutokana na uzoefu wake akafanikiwa kumpoteza yule aliyekuwa akitufuatilia " Si nilikwambia lazima amepandikiza watu wake kila sehemu cha msingi inabidi tutoloke Zanzibar mapema kwa sababu na uhakika kwa sasa atakuwa anajiandaa kuja huku" nikasema " Umejuaje?" akauliza 
" Kwa sababu tumempoteza jamaa yake hivyo atachukia na kutaka kuja kututafuta,inabidi kesho asubuhi sana twende Dar na boti ya kukodi na huko tupande ndege kwenda Mombasa" nikaeleza " Kwa nini Mombasa? Na sio hapa hapa Tanzania?" akauliza " Hapa Tanzania shemeji ana mtandao wake nahisi kila sehemu,sihitaji kukuingiza kwenye matatizo hivyo kubaliana na mimi" nikamwambia Joan hakuwa na cha kusema kwa wakati huo mbele yangu kwa sababu alikuwa akitegemea kila kitu kutoka kwangu Kutokana na uchovu hakuna aliyejishughulisha na mwenzake kabisa,baada ya kuoga tulilala mpaka asubuhi ilipofika asubuhi tulijiandaa na kwenda kutafuta boti ya kukodi ili twende Dar kisha kuelekea Mombasa ili kujificha.
Tulibahatika kupata boti kwa gharama kubwa na ikaondoka na sisi kwenda Dar Hakuna tatizo lolote tulilopata njian mpaka tunafika Dar Nilinunua kofia mbili zilizotusaidia kuficha sura zetu na pia tulivaa nguo na miwani isiyofahamika kwa shemeji Tulichukua gari ya kukodi mpaka uwanja wa ndege na kukata tiketi za kuelekea Mombasa'
 Tulipata ndege inayoondoka asubuhi ya saa nne Tulikaa eneo la kusubiria abiria na pembeni yetu akaja na kukaa akiwa kavaa kofia ya kuficha sura na miwani myeusi pia Muda wa kuondoka ulipofika tulipanda ndege na baada ya muda mfupi ndege ikaiacha ardhi ya Dar " Nashukuru Mungu tumeshamkwepa yule baradhuli" nikasema " Mimi pia na furaha"akajibu 
 Joan " Samahan jaman" sauti ya kike ambayo ni kama tunaifaham ikatushtua Tulipogeuka tukakuta ni yule mdada aliyekuwa kaziba sura yake,, Akaivua miwani na kofia " Mama yangu" akasema kwa nguvu Joan Alikuwa shemeji mwenyewe!!!! " Na nyie mnaenda Mombasa?" aliuliza

INAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.