PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA HAMSINI NA TANO (55)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilipigwa na butwaa kutokana na yale maelezo ya Joan " Na ndiye aliyekupigia anakwambia kuwa ameona damu chumbani kwake?" nikauliza " Ndiyo,jaman Jun nisaide jaman me ntauawa hivi hivi najiona" akasema Nilikaa kitandani kwa dakika kama tano nafikiria nikashindwa kitu cha kuamua " Kwanza katokaje selo?" nikajikuta naongea bila kujijua " Kwa maelezo uliyonipa alivyo gaidi unashangaa imekuwaje akatoka selo? Pole me naondoka hapa Jun sasa hivi asije kuniua" akasema Joan Joan aliposema hivyo tu na mimi nikapata wazo la kufanya pale pale " 
Panga nguo zako tuondoke" nikasema " Unasema?" akauliza " Nimesema panga nguo zako tuondoke" nikamwambia tena " Tunaenda wap jaman si useme?" akauliza " Sirudii tena panga nguo tuondoke" nikasema tena Joan akaondoka na kuanza kupanga nguo zake pale,na mimi nikaondoka na kwenda chumbani kwangu na kukusanya nguo zangu ovyo ovyo kwenye begi na kisha nikachukua kadi zangu na za shemeji kwenye droo za benki nikatoka " 
Uko tayali?" nilimuuliza " Yap niko tayali" akajibu " Nifate" nikamwambia Tukatoka mpaka nje nikataka kuchukua gari ila nikasita na kutoka mpaka nje Nje tukachukua gari ya kukodi " Tupeleke uwanja wa ndege tafadhali" nikasema Muda wote huo Joan alikuwa ananiangalia tu huku akishangaa kila nilichokuwa nakifanya Gari ilienda speed kama tulivyomwagiza dereva " Lakini tunaenda wapi shemeji?" akauliza "

 Naomba kuanzia sasa usiniite shemeji tena,na utajua" nikasema " Sawa nikuiteje sasa?" akauliza " Sijui ila ita jina llote utakalopenda lakin sio shemeji na naomba usiulize maswali mengi mengi" nikamwambia Alinielewa na kunyamaza,muda woote huo nilikuwa nafikilia namna ya kumkimbia shemeji na kuishi mbali naye kwa aman Moyo wangu ulishanasa kwa Joan, nilihisi nampenda kwa kiwango kikubwa sana mpaka hapo sikutaka kumpoteza kabisa na nilikuwa tayali nife ila yeye abaki salama na ndiyo sababu ya kuona bora nitoloke naye " Najua shemeji anaweza kufanya chochote kunizuia ila nitajitahidi kufanya chochote ilimradi niwe mbali na mikono yake" niliwaza 
Kwa bahati nzuri tulipofika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere tulipata ndege iliyokuwa na ratiba ya kuondoka dakika kumi baadae kwenda zanzibar Tulikata tiketi na kukaa sehemu ya kusubiri usafiri " Mungu nisaidie tufanikiwe kutoloka salama" niliwaza Na kweli mungu alikuwa upande wetu na baada ya muda mfupi tulifanikiwa kupanda kwenye ndege na safari ya kwenda Zanzibar ikaanza 
" Joan" niliita " Naam baby" akajibu " Nafikiri huu ni wakati mzuri sana wa kukaa mbali na mikono ya shemeji,nahitaji kuishi kwa amani tena na mwanamke ninayempenda, ndiyo sababu nimeona nikuchukue na kuja huku tujifiche kwa muda wakati tukiangalia cha kufanya" nikamwambia " Na pia nahisi nakupenda sana tena sana mke wangu,nahitaji uwe wangu wa maisha,kwa sasa bora nife mimi ila wewe ubaki salama kwa hiyo nitakupigania mpaka mwisho"nilimwambia Joan aliniegemea kifuani kwa madeko kabisa ya kimapenzi " Ahsante sana Jun, nimeamin unanipenda sana,na mimi naahidi nitakupenda milele" akajibu
 Tuliendelea kupiga story mpaka ndege iliposhuka uwanja wa ndege pale Zanzibar Tulichukua gari ya kukodi na kumwambia atutafutie Hotel ya bei ya kati,isiwe ya gharama sana wala ya bei ya chini sana ili yule nyang'au asitupate Alitupeleka Ukwajuni Lodge kupumzika Ilikuwa ni sehemi iliyotulia kiasi chake Tulichukua chumba na kuingia chumbani kupumzika Joan alitupa mabegi kwenye sofa iliyokuwepo pale na kisha akanirukia na kunikumbatia "Nitakupenda milele mme wangu" akasema Kabla sijajibu simu yangu ililiia mlio wa kuonesha kuna sms imeingia,nikaichukua na kusoma " Kalibu Ukwajuni lodge mme wangu,nimeshaweka oda ya chakula ukishamaliza kuoga njoo tule huku sehemu ya kulia chakula" Sms ile ilitoka kwenye namba ya simu ya shemeji!!! Jasho lilinitoka!!!!

ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.