LEO KATIKA HISTORIA: MIAKA 20 BAADA YA AJALI YA MELI YA MV BUKOBA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
 Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbw pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uhokoaji

LEO imetimia miaka 20 tangu itokee ajali ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Bandari ya Mwanza na Bukoba. Kama zilivyo ajali nyingine nyingi, hii ilipoteza maisha ya mamia ya Watanzania na kuwasababishia wengine hasara ya mali. Umati ulojaa simanzi kwa majonzi na msiba uliosababishwa na ajali hiyo uliahidiwa kwamba Serikali kuanzia wakati huo ingejidhatiti kuchukua hatua za tahadhari za hali ya juu ili kuhakikisha usalama katika vyombo vya usafiri unakuwa si kitu cha kubahatisha, na kwamba hatua madhubuti zitachukuliwa kuhakikisha kuwa ajali zinazozuilika haziwi tena chanzo cha umauti kwa wananchi wa nchi hii. 

Sina hakika na maana ya ahadi hiyo, iliyotolewa kupitia Rais wa wakati huo Benjamin Mkapa na kama ilikuwa ya dhati kiasi gani, na sina hakika vile vile kama ilitokana na kile kisemwacho na wanasiasa mara nyingi kwamba ‘husema wasichokiimaanisha na humaanisha wasichokisema’. Tumekuwa na utaratibu wa kawaida sana kupeana maneno ya faraja na kutafuta visingizo vya harakaharaka kutaka kueleza sababu za kila ajali inayotokea bila kuchukua hatua madhubuti kudhiti ajali hizo, ambazo nyingi zinazuilika.
 Kati ya sababu za kuzama kwa MV Bukoba ni kujaza watu kupita uwezo wake, lakini ugonjwa huu umeendelea kukomaa na kuwa chanzo cha ajali nyingi za majini kama vile hatutajifunza kutoka kwa MV Bukoba.  

Ripiti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.
Kati ya hao 114 waliokolewa wakiwa hai wakati 391 waliokolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na ndugu na jamaa kuzikwa kwao pia Jumla ya miili 332 haikupatikana.
Kila mwaka ifikapo Mei 21 watu mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa dini na mbalimbali kwenda eneo la makaburi na kufanya maombi kwa ajili kumbukumbu ya ndugu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa MV Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa, aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi, ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama kuu ta Tanzania.
Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu),  Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.
Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, MV Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.
Serikali iliahidi kukata rufaa lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.
Kwa kipindi kirefu MV Bukoba ilikuwa ‘kaburi’ lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.
Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji na ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti kwani ilikuwa inakosa uwiano.


Uongozi wa Pamoja Blog unatoa pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza wapedwa wao kwenye ajali ya meli ya MV Bukoba.
Post a Comment
Powered by Blogger.