ISHARA 7 KUWA MUMEO ANAKUPENDA KWA DHATI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


1.    ANAAMILIANA NAWE VIZURI:
Mwanaume anayekupenda anazijali hisia, mahitaji na raghba zako. Anaziona hisia na mahitaji hayo kuwa ni muhimu kama mahitaji yake. Hujali kuhusu ustawi wako na atafanya juhudi ili kuboresha maisha yako. Sio tu kwamba anaamilia nawe vizuri, bali pia ni mwema kwa familia na marafiki zako.

2.    ANAKUPA MUDA WAKE:
Hakubali muda mwingi upite bila kukuona. Unapokuwa na fursa hupenda kuwa pamoja nawe na kutenga muda wa kukaa pamoja. Ikiwa uko mbali huwasiliana nawe, na wakati wa likizo hupenda kuwa pamoja nawe.

3.    WEWE KWANZA:
Wewe ni kipaumbele chake na amekuwa akilini mwake kiasi kwamba huwasiliana nawe mara kwa mara. Anapofanya maamuzi hukufikiria na anajalia kuthamini mawazo unayompatia hata kama hatayafanyia kazi. Anapoongea nawe hutumia “sisi” badala ya “mimi”, na kukujumuisha katika mipango yake ya baadaye.

4.    ANAKUHURUMIA:
Mwanaume anayekupenda sana hufurahia unapopata mambo mazuri. Anakuhurumia unapokutana na nyakati ngumu. Daima yupo nawe katika raha na dhiki.


5.    ANATAKA WATU WAKUJUE:
Anaona fakhari kuwa pamoja nawe na haoni tabu kabisa kukutambulisha na kukusifia kwa watu. Kwenye shughuli za kifamilia hawezi kukuacha nyuma, na husuhubiana nawe katika matukio muhimu.

6.    NI MWAMINIFU:
Ni mwaminifu kwako na kwa uhusiano wako. Hufanya anachosema na hukuweka wazi kama jambo husika hawezi kulifanya. Mambo yanapotokea, huwa na utashi wa kuyakabilia. Japokuwa sio mkamilifu, hujitahidi kuwa mume bora.

7.    HUKUTAKIA MEMA:
Mume anayekupenda hukuhamasisha kufanya mambo mazuri. Hukuhamasisha kuyafikia malengo yako, kwa kutambua kuwa ukiwa na furaha, utamfurahisha.


Huweka uzito kwenye tabia na matendo yake kuliko maneno yake. Tabia na matendo yake yatakuonesha kuwa anakupenda au la. Ni rahisi kwa mwanaume kusema “ninakupenda” kwa sababu hicho ndicho unachotaka kusikia. Mtihani wa kweli wa kujua kama anakupenda ni pale atakapoonesha ishara na alama tulizozieleza hapo juu. Mwanaume anapokupenda, hutahitaji kusikia maneno yake kwa sababu utajua tu.
Post a Comment
Powered by Blogger.