WATU WATANO WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI MKOANI MBEYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Watu watano wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa katika ajali ya basi la HBS eneo la Maji Mazuri, Mbeya Vijijini. Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya mjini kuelekea Tabora kuitia Chunya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala aliyekuwa kwenye shughuli za kusimamia usafi ameenda kwenda eneo la tukio ili kusaidia uokoaji.
Akizungumza baada ya kutoka eneo la tukio, amesema waliofariki dunia ni wanaume wawili na wanawake wawili na mtoto mdogo, ambao bado majina yao hayajatambuliwa na majeruhi ni 29.
Taarifa za awali inadaiwa ajali hiyo imesababishwa na gari kufeli breki na kisha kugonga gema na kupinduka. Dereva aliruka na kutokomea kusikojulikana.
Post a Comment
Powered by Blogger.