TFF YALAANI VURUGU ZA MASHABIKI WA TIMU YA SIMBA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

TFF imesikitishwa na kitendo hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba SC, na kusema inalaani kitendo hicho ambacho sio cha kiuana michezo, huku ikiwataka wanachama, washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kama kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika vilabu vyao.

Mashabiki wa klabu ya Simba walifanya vurugu kwa kurusha mawe, wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji, magari waliyokuwa nayo baada ya timu yao kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans kwa bao 1- 0.
Jeshi la Polisi baada ya kuwasishi mashabiki kuondoka eneo la uwanja punde tu mchezo ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea kurusha mawe hali iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya katika eneo hilo.
Kufutia kitendo hicho, Jeshi la Polisi lilihakikisha bus la timu ya Simba SC na viongozi wake wanaondoka salama uwanjani baada ya kuwatawanya mashabiki hao, kwa kupitia mlango wa karakana ya wachina waliojenga uwanja huo.

Aidha TFF imeviomba vyombo vya Usalama na Ulinzi kuwachukulia hatua kali mashabiki waliohusika na kitendo hicho, kwani kufanya vurugu ni kosa la jinai na wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Post a Comment
Powered by Blogger.