MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» »Unlabelled » SERIKALI YAKIRI KUDAIWA SHILINGI 67.3 BILIONI NA WALIMU


Pamoja Blog 4/23/2016 11:00:00 AM 0

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Serikali imesema bado inadaiwa na walimu deni linalofikia Sh67.3 bilioni, ikiwamo mishahara.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jaffo alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Aida Khenani bungeni.

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kumaliza madai ya walimu ya muda mrefu nchini.

Pia, alihoji kuhusu madai ya walimu waliosahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka jana ambao hawajalipwa hadi sasa.

Naibu Waziri huyo alisema Serikali imeendelea kulipa madeni ya walimu kupitia mamlaka zake kila yanapojitokeza.
“Mfano, Oktoba 2015, Serikali ililipa Sh20.1 bilioni na Februari mwaka huu imelipa Sh1.17 bilioni za madeni ya walimu nchi nzima,” alisema Jaffo.


Alitoa mchanganuo kuwa kati ya kiasi kinachodaiwa, alisema Sh17.5 bilioni ni madeni yasiyo ya mishahara wakati madeni ya mishahara yanafikia Sh49.8 bilioni ambayo kwa pamoja yanafanyiwa uhakiki.

Kuhusu malipo ya walimu waliofanya kazi ya kusahihisha mitihani alisema baadhi ya mikoa haijapeleka madai yao hadi sasa licha ya kuwa mwisho wa kupelekwa ilikuwa ni Aprili 15.

Alisema mikoa tisa tu ndiyo ilipeleka na kuitaja kuwa ni Mbeya, Mara, Tanga, Arusha, Kigoma, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Iringa.

Alisema madeni hayo ya mikoa hiyo yanahakikiwa ili walimu walipwe.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments