PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA TISA(39)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Yule mzee ambaye alikuwa ndugu wa ukoo wa baba ambaye mimi sikujuana naye sana alitilia mashaka kilichokuwa kikiendelea pale kati yangu na shemeji Alipotoka pale alirudi eneo walilokaa watu wengine lakini macho yake yakawa yanacheza kutoka kwangu kwenda kwa shemeji,alijitahid kutufatilia ili agundue chochote kinachoendelea kati yetu. " Hawa watu si bure! Mbona huyu kijana ni kama ana mawazo saana?
 Na akili yake ni kama haiko msibani? Na yule mkwe mbona analia watu wakiwa naye busy? Na anawasiliana sana na simu? Hapana" alijisemea yule mzee " Vip mzee mwenzangu? Umeanza kuhalibikiwa kama vijana wa kisasa wanavyodai?" mzee mmoja aliyekuwa kaketi jilani naye akamuuliza " Unasemaje?" akauliza kwa mshtuko na hamaki " Nakuona muda mrefu unaongea mwenyewe nashangaa mzee mwenzangu" akasema " Aaaah! Hapana ila kuna kitu kinanichanganya" akajibu yule mzee " 
Sema mzee mwenzangu? Yawezekana nikawa na wazo zuri na kujenga mawazo yako" akajibiwa " Twende pembeni" akasema "Sikia hapa kuna kitu nahisi hakipo sawa" akasema mzee wa kwanza " Kivip?" akajibu mzee wa pili maarufu kama Urio " Sikia Urio,hawa wenye msiba siwaelew elew,nimemkuta mkwe wetu na shemeji yake wanazozana sana na nilipojalibu kuwadadisi nikagundua hakuna maelewano sasa haya mambo kiukoo si sawa,ila pia nimamfatilia mama mzazi wa marehem na yeye naona hayuko sawa" akasema Mushi " Mmmmmh! Mbona sijakwelewa?" akasema Urio "

 Sikia nataka unisaidie,naomba tuwafatilie hawa watu watatu nyendo zao wote,na hasa wanapokutana wenyewe kwa wenyewe,nahisi kuna jambo zito limejificha hapa katikati" akasema Mushi " Aaah! Kama ni hilo aisee halina tatizo kabisa et! Me nikigundua kitu aki ya nan yesu na maria lazima nikwambie" akasema Urio Wale wazee wakaondoka na kurudi maeneo yao huku wakiendelea kufatilia nyendo zetu. 
Siku hiyo tulilala kwa amani na hakuna kati yetu aliyewasiliana na mwenzake. Asubuhi ya siku iliyofata ambayo ilikuwa ndiyo siku rasmi ya mazishi ndipo kizazaa kilipoanzia Muda wa saa mbili mama aliwakwepa wazazi wenzake na kunifata " Mwanangu Jun" akasema " Naam mama" nikajibu " Naomba kuongea na wewe pembeni kidogo" akasema mama " Haina shida" nikamjibu 
Nilinyenyuka na kuwaaga wale vijana wenzangu niliokuwa nimekaa nao kisha nikamfata mama Uzuri wa kule kwetu uchagani kuna migomba mpaka kalibu na nyumba kabisa hivyo tulielekea migombani ili tupate faragha 
Kumbe wakati mama ananyenyuka kunifata Urio alimuona na akamfatilia " Mwanangu narudia tena kukuonya usije ukasogea eneo la kaburi utakufa mwanangu,kumbuka nimebaki na wewe peke yako mwanangu" akasema mama " Usijal mama sitaenda" nikajibu " Lakin pia nakuomba mwanangu,kaa mbali na huyu mwanamke,sio mtu mzuri kabisa,najua unaniogopa ila elewa nipo na wewe nahitaj baada ya msiba tuongee mimi na wewe kama mama na mwane kisha tujue namna ya kumuondoa huyu mwanamke kwenye maisha yetu" akasema mama kwa hisia saana " 
Usijal mamamngu" nikamjibu Kitu ambacho hatukuwa nacho makini ni choo iliyokuwa nyuma yetu,kumbe mzee Urio alikuja na kusimama nyuma ya zile choo kisha akatusikiliza kila kitu Aliondoka pale na kumfata mzee Mushi " Aisee mzee mwenzangu kumbe ulikuwa unaongea ukweli,hapa kuna tatizo tena tatizo lenyewe ni kubwa sana" akasema Urio " Kivip? Umepara nini tena?" akauliza Mushi " 
Nimemfatilia yule mama,akaenda na kumchukua kijana wake kisha wakatoka kwenda chemba,nikawafatilia na kusikia yule mama akimzuia mwanae asiende kwenye kaburi la kaka yake na pia wamemwongea vibaya mkwe" akasema Urio " Aisee si nilikwambia! Sasa kwa kawaida mtu asipoenda kwenye kaburi la ndugu yake wakati wa maziko si huwa anahusika na kile kifo? Yesu na maria watakuwa wamemchukua et?" akaongea kwa mshangao " Kumbe??? Hapa lazima tuwaumbue! Haiwezekani!" akajibu Urio

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.