PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA NANE (38)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Mjomba aliendelea kutuita ili tuingie kwenye gari na kuendelea na safari na mama akageuka na kuelekea magari yalipo. Niliduwaa pale kwa muda kisha na mimi nikaunga tela na kupanda gari nililokuwa nimepewa siti ya kukaa tangu mwanzo. Safari iliendelea huku nikiwa mwingi wa mawazo sana,sikujua hatima ya lile sakata ni nini? Na hata mimi mwenyewe nilianza kujishangaa ilikuwaje nikaweza kutekeleza kitendo cha kinyama kiasi kile. 
Tulifika Moshi mjini mida ya saa saba za mchana na kushika barabara ya Mwika kuelekea Moshi vijijini eneo la Kibosho umbwe pembeni ya shule ya Somsom ambako ndiko nyumbani kwetu halisi. Baada ya kuingia eneo la migomba linaloelekea nyumbani akina mama wa kijijini pale na ndugu kadhaa walitupeokea kwa vilio sana mpaka wakanipa majonzi makubwa Nikaanza kujihisi hatia kubwa sana juu ya kitendo nilichokitenda "
 Hivi kwa nini nimefanya vile? Ni kitu gan hasa kilichonisukuma kufanya vile? Au shemeji kuna kitu alishanifanyia bila kujijua? Aaaah! Potelea mbali maji yameshamwagika sina cha kufanya" niliwaza huku nikipambana na ukweli halisi wa lile tukio Niliposhuka kwenye gari wakati mama amejichanganya na akina mama wenzake wakilia na kumfatiji niliondoka na kutafuta shemeji alipo. Nilimkuta Shemeji amekalishwa na mawifi nao wakijalibu kumfariji huku na yeye akilia kiuongo na kweli ili watu wasimshtukie,nikamshika mkono
 " Samahan jaman na shida naye kidogo tafadhali" nikawaambia Nilimvuta shemeji kuelekea kwenye migomba eneo la mbali kidogo ili watu wsitushtukie " Mwenzangu maji yameshamwagika" nikamwambia "
 Inabidi kuyaoga " akajibu kinyodo " Me naongea serious ila wewe unafanya matani?" nikawa mkali " Una maana gan kwan baby?" akasema " Sikia shemeji,mama anajua kila kitu kinachoendelea" nikamwambia " Sijakwelewa,!!! Anajua nini tena? Na nini
kinachoendelea?" akahamaki " Ni hivi leo wakati tukiwa mombo,mama aliniita na kunieleza kila kitu ambacho tumekifanya" nikasema Shemeji alishtuka na hilo nililiona dhahiri sema hakutaka nijue kama kashtuka akajikausha " Imekuwaje akajua?" akauliza " 
Unakumbuka ile line niliyokwambia kuwa niliidondosha akaiokota?" nikamuuliza " Ndiyo" akajibu " Sasa siku ile kumbe wakati naruka ukuta ili kuondoka alikuwa anaanua nguo za kumbadilishia kaka kule nyuma akaniona na baada ya hapo akawa na wasiwasi na mimi ndipo alipoenda kuikagua ile line na kuona kila kitu" nikaeleza 
Shemeji alitulia kwa muda akiniangalia sana ,nilichompendea shemeji ni akili,alijua kukabiliana na tatizo kwa haraka sana " So wewe una wazo gan hapa?" akaniuliza " Me na wazo gan zaidi ya kuchanganyikiwa" nikajibu " Sasa wewe ni mwanamme wa aina gan? Mwanamme suruali? Tatizo likikukuta huwez kupata suluhisho bali unachanganyikiwa?" akafoka " Samahan ila me inabid tumtafute mama tuongee naye yaishe na yeye akaushe" nikajibu " Weeeeeee! Thubutu! Sikia uchungu wa pilipili haumzuii mlaji sawa" akajibu " Una maana gan?" nikamuuliza " Namaanisha yeye si pilipili kwenye chakula? 
Sasa tuondoe sehemu yenye pilipili kwenye chakula ili tuendeelee kula vizur" akasema kwa kujiamin " Sijakusoma ujue? Una maanisha tumuondoe mama?" nikasema kwa mshangao " Hilo sio swali labda uulize swali" akajibu kwa nyodo " Wewewewewewewe! Hapo ntakupinga mpaka kesho, nimebaki na mama peke yake,baba alikufa,kaka nimemuua mwenyewe na kwetu tulikuwa wawili af nimuue na mama? 
Unataka nibaki mwenyewe? Hapo NO tena big NO" nikajibu kwa hasira Kuna mzee mmoja alituona kama tunajibizana vile akatusogelea " Kuna nini jama? Mbona kama mnazozana?" akauliza " Aaah! Hapana baba hatuzozani ila kuna vitu namwelewesha shemeji hapa" akajibu shemeji " Aaah! Jaaman mbona dhahiri shahiri inaonesha kama mzozo?" akauliza tena " Samahan jaman naomba niwaache " nikasema kwa hasira kisha nikaondoka Shemeji alimwelewesha yule mzee mpaka akamwelewa na kisha akaondoka Kumbe yule mzee alibaki na maswali kichwani juu ya tukio lile!!!

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.