PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA SABA (37)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka sana kusikia mama ananieleza habari ile ambayo sikutarajia kabisa kama atakuwa anaijua “ Unaongea nini mama? Mbona sikuelewi?” nikamuuliza “ Unasema hunielewi? Basi endelea kubisha tuone tatizo litaamkuta nani kati yangu na wewe”akasema Katika hali halis nilikuwa nimeogopa kupita maelezo nilihisi kijasho chembamba kikinitoka gkwenye uti wa mgongo kushuka mpaka makalioni. 
“Lakini mama kumbuka mimi ni mwanao sasa hayo mambo ya uongo unayoongea watu wakiyasikia huoni kama utaniweka kwenye wakati mgumu?”nikajitia kuuliza kwa hasira “Sikia wewe mpuuzi,mimi nilizaa watoto wa kiume wawili peke yake,wewe na kaka yako,nilitegemea muishi kwa amani na upendo na kusaidiana matokeo yake yamekuwa kuuana?!! Hata siamin,nahisi hata ile ajali haikuwa ya kupenda kwa mungu bali ni mpango wa binadam,nasubiri msiba uishe ili unieleze vizuri”alifoka mama 
Nilitetemeka kabisa kiasi cha kuonekana dhahiri machoni pa mama “ Kama haukumuua kakako unatetemeka nini sasa?”akauliza na mimi sikuwa na cha kujibu ikabid nitulie kama sielewi kinachoendelea “Sikianiliporudi kutoka dukani nilikuta line ya simu pale chini wakati naondoka nilifagia chumba kile na sikukuta kitu kama hicho,nilishtuka na kujua kuna kitu kinaendelea pale ila sikujua ni nini? 

Nilitoka ili nikamuulize mlinzi kama aliona mtu akiingia ndani,alipojibu hakuona nikasikia kishindo cha chombo kikianguka ndani,nikazunguka kwenye maua pale ili nianue nguo ya kumbadilishia kakako ndo nirudi ndani,ndipo nilipofanikiwa kukuona ukiruka ukuta,nilishangaa sana kwa nini uruke ukuta? Kurudi ndani nikachukua simu yangu na kuweka line yako nikaziona message zako na mpuuzi mwenzio”akasema mama 
Nilikuwa mdogo kama piriton mbele ya mama!sikuwa na ha kuongea tena kwa sababu ukweli ulikuwa umeshawekwa wazi kabisa “ Jaman tunaondoka hivyo,tunaomba kila mmoja apande kwenye gari ili safari iendelee”aliongea mjomba kwa sauti Nikageuka kumwangalia mama “Sikia tukifika kibosh lia sana na ujifanye unapoteza faham ili wasije wakakulazimisha kulikalibia kaburi la marehemu,kumbuka ukikanyaga pale ndo kifo chako,nimbakiwa na kijana mmoja peke yake,sitaki kukupoteza ma wewe”aliongea kwa msisitizo mama Nilitishika sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ITAENDELEA JUMAPILI
Post a Comment
Powered by Blogger.