PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA SITA (36)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka kuona mama ananiangalia kwa jicho baya vile ila nikajikausha kama sijamuona " Mama poleni sana hii ni hali ya kawaida sana na inawatokea wengi,naomba niwaache mkiendelea na taratibu za kawaida za kuaandaa msiba" akasema yile jamaa ambaye alikuja kama Dokta " Sasa wewe Dokta mbona haushauli chochote kuhusu marehem?" akauliza mama " Kivip mama?"jamaa akauliza " Mfano apelekwe mochwari unataka tuishi nye humu ndan?" " aaaah! Samahan mama nimepitiwa,ndiyo mnapaswa mmepeleke akachomwe dawa za usingizi nma kutunzwa wakati taratibu za msiba zikiendelea" akasema jamaa
 Wakati huo shemeji aliendelea kulia kwa nguvu hali iliyosababisha majirani waanze kujazana pale " Beba majukumu ya kiume Hun" akasema mama akiwa haniangalii usoni Nilitoka na kuingia ndani nikabadili shati na kuvaa t shirt yangu nyeusi kisha nikatoka mlangoni nikakutana na mama " Heeee! Mwenzetu ulishajiandaa kwa msiba tayali ee? Mbona nguo mpya kabisa hiyo?" akauliza kisharishari " Hapana mama,niliinunua zaman sema nilikuwa siivai" nikamjibu na kupitiliza nje, 
Nilikutana na majirani zeti wakiume na kushauriana tuupeleke mwili wa marehemu mochwati,waliingia na kunisaidia kubeba kisha tukaweka mwili kwenye gari na kuondoka kuelekea Muhimbili huku nyuma tuliacha shemeji akitulizwa na akina mama " Mme wangu eeeee!!....mmme wangu umeniacha bado mdogo....umeniacha mbali mme wangu....hujaniachia hata mtoto wa ukumbusho jaman....mme wangu si bora ningetangulia mimi badala yako? .....kila mmoja wetu alikutegemea jaman" alilia sana kiasi cha kuwaliza na wenzake waliokuwa wakimpooza Tulipofika hospitalini tulipokelewa na kulipia gharama zilizokuwa zikihitajika na kisha tukaacha wakiendelea na taratibu zao sisi tukarudi nyumbani.

Nilipofika nilimkuta mama na yeye ameshikwa na uchungu analia sana kiasi cha watu kushindwa kumpooza Nilienda na kukaa sehemu ya wanaume kisha tukapiga soga za kupoteza muda Jioni ya siku hiyohiyo wagemi ambao ni ndugu zetu walianza kuwasili pale nyumbani na hali hiyo ikasababisha tukae kikao cha ukoo ili kuamua pa kuzikwa kaka "
 Jaman nafikiri kila mmoja amefika hapa akijua yaliyotukuta,kwanza poleni" aliongea baba mdogo wa Kinondoni " Ahsante" wakajibu " Kikao chetu ni kifupi na ni cha kuamua sehemu maalum ya kuzikwa kijana wetu kati ya kijijini kwetu Kibosho au hapahapa Da" akasema " Hakuna utaratibu katika kabila yetu sisi wachaga ya kuzika mtu tofauti na nyumbani kwao na isitoshe kijana wetu alishajenga mji wake pale Somsom hivyo lazima akahifadhiwe kwake" akaongea mjomba "
 Jamani hilo no wazo la mjomba wa marehemu sijui wengine mnasemaje?" akauliza bandogo " Sidhani kama hilo linahitaji mjadala la msingi ni utekelezaji jaman au kuna mtu anabisha?" akauliza ndg mwingine " Hakuna" wakajibu " Basi kwa kutokana na maongezi niliyoongea na mdogo wa marehem mpaka sasa mambo hayajakaa sawa,marehemu aliibiwa kiasi kikubwa sana kwenye ajali na pia acc zake benk hazijatolewa ruhusa ya kutumia hivyo naomba tutoboke kidogo ili mambo yaende sawa" akasema bamdogo 
Mama alinipiga jicho kali sana kwa mara nyingine nikaangalia pembeni. Michango ilitolewa na kisha taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Kibosho umbwe kwa ajili ya mazishi zikaanza Asubuhi ya siku iliyofata ndipo msafara ulipoanza kuelekea Moshi kwa ajili ya msiba Msafara ulikuwa mkubwa hasa kutokana na kaka kuwa na marafiki wengi sana kibiashara Dar Tulifika Mombo saa sita za mchana na kushuka ili tupate chakula na cha kushangaza mama akanishika mkono na kunivuta pembeni " Sikia,taratibu zetu wachaga ni kuwa ukimuua mtu usisogelee kaburi lake wakati wanazika hivyo kuwa makini sana Jun,sitaki niwapoteze wote" alinambia Nilitumbua macho kwa mshangao!!!!

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.