PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA TANO (35)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilitulia pale chumbani nikisubiria muda wa kufanya like tukio aliloniagiza shemeji ufike ili nilitekeleze niondoke bila kushtukia " Niko ndani nasubiri muda nifanye yangu" nilimtumia sms shemeji " Poa ngoja nimuondoe mama ili umalize kazi" akanijibu kwa sms Muda si mrefu nilisikia simu ya mezani kule sebuleni ikiita na baada ya muda nikamsikia mama akitembea kuelekea sebuleni " Haloo.....Ndiyo mama.....hapa dukan ee?....sawa mamangu...sawa" aliongea mama na moja kwa moja nikajua kuwa alikuwa akiongea na sheemeji Muda mfupi mesage iliingia kwenye simu yangu " Mama anaondoka hapo muda si mrefu kwenda kwa Mangi kuchukua mkate atakaonywea chai hivyo maliza kazi" 
Niliielewa ile sms ilikuwa ina maanisha nini ila nilijikuta ujasiri wote ukinitoka na kubaki nikitetemeka Kweli dakika chache baadae nilimsikia mama akifungua mlango wa kutoka nje na kutoka nikaenda na kuchungulia nikamuona akifungua geti na kwenda nje. Nilirudi ndani na kukimbilia chumbani kwa kaka na kuchukua mto aliokuwa amelalia kisha nikamfunika nao usoni. Kazi ilikuwa nyepesi sana kwa sababu kaka hakuwa na faham kabisa hivyo alitapatapa kwa muda mfupi kisha akatulia 
Nikaaangalia kama kweli ameshakufa au la!? Nilipohakikisha amekufa nikaurudisha ule mto ulivyokuwa kisha nikajiandaa kuondoka Pale pale nikasikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa ikanibidi nizame uvunguni kwani nisingeweza kuwahi kutoka Kweli mama aliingia pale chumbanina kumuangalia mgonjwa,hakuelewa chochote kwa sababu alimuacha kaka akiwa hana faham na pia akamkuta akiwa kimya vile vile " 

Mmmmmh! Hii si ni laini ya simu? Ni ya nani tena? Mbona haikuwa hapa chini wakati naondoka?" aliongea mama akiiokota Nilitetemeka sana kugundua kuwa wakati nafanya lile tukio line yangu ya simu iliyokuwa kwenye mfuko wa shati ilidondoka bila kujua na mama aliiokota Mama aliondoka na kwenda nje ili kumuuliza mlinzi kama kuna mtu ameingia na mimi nikatumia wakati huohuo kutoloka na kwenda chumbani kwa sheemeji. Nilipitia mlango wa nyuma na kuruka ukuta kama mwanzo na kisha nikaondoka eneo lile.
 Nilitafuta bajaji na kukodi kisha nikaondoka kuelekea kazini katkati ya mji Nilipofika nilimweleea shemeji kila kilichotokea " Una uhakika hujamgusa kwa namna yeyote ile usije ukawa umeacha alama za vidole?" akauliza " Nina uhakika huo sema kuna tatizo dogo limejitokeza" nikamwambia " Tatizo gani tena?" akauliza " Wakati nimejificha uvunguni mama aliingia na kuokoya line kumbe wakatai nafanya tukio nilipoteza line yangu pale" nikasema Shemeji alitulia kwa muda akitafakari sana juu ya lile "
 Dah! Angekuwa mpelelezi tungeshasema tumekwisha sema mama!!!!! Mmmh! Tuombe Mungu" akasema shemeji Tulituilia na kuendelea na kazzi za pale dukani kwa muda wa saa mbili ndipo simu kutoka kwa mama ikaingia " Ndiyo mama....unasema?......imekuwaje tena?.....umejuaje?...subiri nimpigie Dokta tuje naye....sawa mama usiwe na wasi wasi ni mzima huyo...sawa" aliongea kisha akakata simu " Yameshasanuka" alisema shemeji 
Alinyenyua simu kisha aakampigia Dokta wake wa magumashi na kumwambia pa kukutana tuelekee home Tulipokutana safari ya kwenda home ikaanza. Tulipofika tulimkuta mama akilia sana pembeni ya kitanda cha kaka Jamaa akachukua vifaa na kupima kwa muda kisha akavitoa " Poleni sana jaman,mwenzenu hatunaye tena" aliongea Pale pale shemeji akaangua kilio hasa,cha ajabu mama hakulia ila nilipomwangalia nikakuta na yeye akiniangalia kwa jicho baya sana mpaka nikashtuka!

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.