PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA NNE (34)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Baada ya yule msaidizi wa kazi kufika alimfata shemeji dirishani " Naam dada?" akasema " Fungua mlango huko nyuma uingie" akaongea shemeji bila kumuangalia Yule mdada wa kazi alifungua mlango na kisha akaingia na shemeji akapandisha vioo vya gari Baada ya kuingia ndani,nilitoa lile kopo la dawa kisha nikageuka nalo na kumpulizia usoni "
 Nini tena jaman? Aaaagh!" aliongea na kutoa ukelele kisha taratibu akaanza kupoteza uwezo wa kupambana na ile dawa na mwishowe akalegea na kuangukia kwenye ile siti ya pale nyuma " Tayali ondoa gari" nikamwambia shemeji na yeye akageuka na kumwangalia kisha akawasha gari Tuliondoka eneo lile kuelekea kwenye kambi yetu ya kule Kimara tulikomuacha kaka na ile maiti ya Dokta
 Tulichelewa sana kufika kutokana na foleni kubwa iliyokuwa barabarani. Tulipofika moja kwa moja tulipiliza ndani na kumkuta Mussa akiwa anatusubir " Kwenye gari kuna boya mwingine anayeweza kutuletea matatizo naomba ukamlete hapa" shemeji alimwambia Mussa Mussa aliondoka na kumleta yule binti wa kazi " Mussa mmalize huyu akiwa usingizini kwa sababu tukimwacha anaweza kuja kuwa shida na kikwazo kwenye njia yetu" akasema shemeji 

Tulimbeba Kaka mpaka kwenye chumba maalumu na kumfanyia usafi wa mwili kisha shemeji akatoka na kununua bandeji tukavifunga vidonda vya kaka kisha tukampakia kwenye gari na kuondoka Safari ya moja kwa moja mpaka Nyumbani na kumkuta mama akitusubir Tulimbeba Kaka na kumuingiza ndani kwenye chumba cha wageni tukamlaza " Jaman mwanangu,kila mtu anakutegemea wewe tafadhali usife mwanangu,utaniacha kwenye hali mbaya sana mamako! 
Tafadhali baba usife" aliongea mama huku akilia Shemeji alimfata na kujalibu kumbembeleza mama ila ilikuwa kama anamwongezea speed ya kulia ikabid amwache na kutoka. Shemeji alirudi baadae na maji ya drip kama zile za Hospitalin kamfungia kaka,kisha akaniita chumbani kwake " Huyu mama hawezi kuondoka leo au kesho na sisi tunahitaji kummaliza huyu ili tubaki huru tufanyeje?" akaniuliza " Yaaan hapa nilipo kichwa hakisomi kabisa shemeji" nikasema " Weee vip? Unafikiri kuwa mwanamme ni kuvaa suruari pekee? Lazima uumize kichwa bwana" akasema kwa hasira " Sasa mbona unanitukana?" nikamuuliza " 
Sikutukani ila nakwambia,umiza kichwa basi" akasema " Ok,una wazo gani?" nikamuuliza Shemeji aliniinamia kisha akaninong'oneza kitu ambacho kilinishtua sana " Haaaaaaaaah! Sa nani atafanya hiyo kazi?" nikamuuliza " Utaifanya wewe mwenyewe" akajibu " Aaaaaah! Me siwezi bana tafadhali sana" nikajitetea " 
Hilo swala halina mjadala,ni lazima ufanye hivyo" akasema shemeji " Sa mbona unaniburuza kwenye maamuzi?" nikauliza " Sikuburuzi ila tunashilikiana" akasema Tulipomaliza maongezi yetu na kukubaliana tuliondoka na kuendelea na majukumu kama kawaida " Yule binti wa kazi yuko wapi jaman?" aliuliza mama " Kwani hajarudi hapa?" akauliza shemeji " Tangu mmeondoka naye sijamuona" akajibu mama "Tumefika hapo dukani na kumnunulia vitu vya chai akarudi" akasema shemeji " 
Basi sijamuona" akasema mama " Huyu binti itabidi nimuachishe kazi huwa ananitoloka na kwenda kwa wanaume na kulala huko akirud anaomba msamaha namsamehe ila leo sitamsamehe" akalalama shemeji Siku mbili zilipita tukiwa vizuri bila kushtukiwa na mtu yeyote yule na mama alikuwa habanduki kitandani kwa kaka,alimsaidia kwa kila kitu huku kaka akiwa hana fahamu 
Siku ya tatu tulipotoka na shemeji alinishushia getini kisha nikaruka ukuta na kuingia ndani kwa kutumia mlango wa nyuma na kujificha chumbani kwa shemeji bila mama kujua Nilitulia mle ndani nikisubir wakati ufike nikamilishe kazi yangu niliyoagizwa na shemeji Ila nilijihisi kutetemeka mwili mzima!

ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.