PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA TATU(33)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka sana kusikia mama kaingia asubuh yote hiyo wakati hata kuamka hatujaamka. Nilinyenyuka fasta na kuvaa flana yangu nikajikuta nimeigeuza nashangaa hata shemeji hakuona hilo kisha nikawahi kutoka na kuingia chumba cha wageni Nilikaa dakika chache niliposikia mama ananiulizia nikaamka kama ndo ninaamka na kuelekea sebuleni " Shikamoo mama" niliamkia " Marhaba mwanangu za hapa ?" akauliza " Za hapa sio nzuri mama kama ulivyosikia" nikajibu huku nikijifanya kuwa na majonzi "
 Pole baba,lakin mbona hamkunipa taarifa? Mpaka napigiwa simu na yule ndugu yenu anayeishi tabata" akasema mama " Tusamehe mama tulichanganyikiwa" akadakia shemeji " Haya,vip mwenzenu? Yuko wap? Na anaendeleaje?"akauliza " Mmmmmh! Bado hali yake ni mbaya,hivi tunajiandaa kumfata tumrudishe nyumbani kwa sababu madaktari wameshindwa na wamesema anapaswa apelekwe nje ya nchi" akasema tena shemeji " Jaman sasa ndo tutafanyaje? Na hiyo pesa ya kumpeleka huko mnayo?" akauliza mama " 
Mmmmh! Yaan hapa ndo maana tukasema tumechanganyikiwa mama,kwa sababu mme wangu alichukua pesa kalbia yote na akaondoka nayo kwenda kuchukua mzigo ,hao wenzake walimshaur abebe nyingi ili wampe mzigo mkubwa tupanue biashara,alivyopata ajali yote iliibiwa" akasema shemeji " Mungu wangu,siku ya kufa nyani miti yote inateleza,na kwenda nje ni kias gan?" akasema mama " Ni gharama mama,nasikia zaidi ya million thelathini" akasema shemeji bila kuwa na uhakika " Jaman mwanangu atakufa namuangalia ndani " akalalama mama "
 Shemeji jiandae tukamfate kwa sababu Dokta ameshanipigia simu" akasema shemeji Mama alijiiinamia pale kwenye sofa na kulia kilio cha kiutu uzima taratibu sana mpaka nikamwonea huruma " Mwanangu kwa nini nisingekufa mimi wewe ubaki?
Tulikutegemea wewe,umeleta mabadiliko kwetu! Mungu badilisha maamuzi sasa" alikuwa akilalamika Nilitoka na kuelekea kwenye kile chumba changu ch nje na kunawa uso isha nikajiandaa kwa safari hiyo ya shemeji Baada ya dakika chache tulikuwa tumeshajiandaa ili kuondoka " Mama ngoja sisi tumfate kaka basi" nikamuaga " Naomba niongozane na nyie jaman" akasema mama huku akinyenyuka na kufunga kitenge chake vizur " 
Aaah! Hapana mama,pale hospitalin hawaruhusu kulia,najua ukimuona utapatwa na majonzi utalia utupe kesi tena,we subiri mamangu" akamuwahi shemeji aliposhtuka kuwa mwili wa kaka haukuwa hospitalin bali kule mafichoni " Jaman! Haya basi" akasema mama kwa style ya kulalamika Tulitoka na shemeji kisha tukapanda kwenye gari ili tuondoke " Tukicheza hapa mambo yataharibika" akasema shemeji " Kwa nini unasema hivyo?" nikamuuliza " Tunamuacha mama na yule housegirl unafikili hatasema?" akauliza " 
Dah! Hilo nalo tatizo,basi mwite mama twende naye" nikasema " Tatizo lako kichwa chako hakifikirii vizur,tukiondoka na mama mwili tunaufata hospitalin?" akauliza tena " Tunafanyaje?" nikauliza Shemeji alifungua sehemu flani kwenye gari yake na kutoa kopo kama la rungu dawa ya mbu na kunipatia " Shika hii,namwita yule demu,akifika nitamwambia aingie kwenye gari,akishakaa siti hizo za nyuma geuka ghafla kisha mpulizie hii dawa ya usingizi kisha tutaenda kumuuliza kule dokta aliko" akasema Nilimwelewa vizuri sana shemeji,nikalichukua lile kopo na kulificha chini ya siti yangu Shemeji alitoa simu na kupiga " Marry...njoo mara moja kwenye gati" kisha akakata

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.