PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA THELASINI NA MBILI (32)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.CURRENT DAR ES SALAAM 
Baada ya shemej kunikabidhi ile siraha ndo iliyofungwa kifaa cha kuzuia sauti isitoke nilijihisi mwepese na mwenye hamu ya kufanya mauaji. Nilielekeza ile silaha kwa Dokta na kisha taratibu nikabonyeza kitufe cha kuruhusu risasi itoke kwenye silaha Risasi nne zilitua kwenye kichwa cha yule Daktari na akanyamaza kimya huku kichwa chake kikiwa kimeachama na kuumwaga ubongo wake nje " Paa...paaa....paaa" shemeji alinipigia makofi "
 Wewe ndiye mwanamme niliyekuwa namhitaji katika maisha yangu,mwanamme asiyeogopa kufanya chochote kwa ajili ya faida yake" akasema " Sio faida yangu pekee baby wangu bali faida ya wote mimi na wewe" nikamjibu " Haya mme wangu faida yetu sote" akasema Wakati tunarumbana simu ya shemeji ikaita na yeye akanionesha ishara ya kukaa kimya "
 Haloo mama.....ndiyo......si nzuri....yah ni kweli kama ulivyosikia.....yaan hapa nilipo nimechanganyikiwa kabisa,Muhimbili wameshauri tumpeleke India na pesa nyingi aliibiwa wakati anapata ajali...ndiyo mama...haya kalibu"akamaliza " Vip? Kuna nini tena?" nikauliza " Mamamkwe" akajibu " Mama yangu?" nikauliza " Ndiyo" akajibu " Anasemaje? Maana na yeye naye mmmh! Hajambo kwa maneno" nikauliza " 
Ameniuliza kuhusu kaka yako,sijui nani kampelekea umbeya tena,ila umesikia nilivyompanga kwa hiyo huyu jamaa hakuna haja ya kumuua,kwa sababu wanakuja kumuona,cha msingi tumwache kwa sababu hali yake ni mbaya ila wakiondoka tu tunamwondoa" akasema " Aaaah! Me nilitaka nimwondoe sa hivi bana atatuzibia baby" nikalalamika "

 Hapana, tufanye vitu kwa akili,ukimwondoa tutakamatwa,acha mama aje amuone hali aliyonayo ila akija tujifanye hatuna pesa na hali ni mbaya kwa sababu nimemweleza kuwa pesa iliibiwa ili akiondoka tummalize jamaa" akajibu Tulimbema kaka akiwa kwenye ile hali yake ya kupoteza fahamu mpaka kwenye gari kisha safari ya kurudi nyumbani ikaanza Tulipofika nyumbani tulimbeba kaka na kumpeleka chumba cha wageni kisha shemeji akatoka kidogo na aliporudi baadae alikuwa na maji na vifaa vya kufungia mgonjwa akamuwekea kaka,na akawa kama amelazwa kabisa Tuliingia kulala ila siku hiyo hatukuwa na hamu ya kufanya mapenzi kutokana na kusikia kuwa mama anakuja " Baby inabidi tumwondoe huyu binti wa kazi" alitoa wazo shemeji "
 Kwa nini baby?" nikauliza " Kwa sababu anajua kinachoendelea hivyo anaweza kuwa mwiba kwetu siku zijazo" akasema shemeji " Kwa hiyo unamrudisha kijijini kwao lin?" nikauliza " Sio kijijini kwao,namaanisha tumuue" akasema shemeji " Kwa nini? Kwani ana tatizo?" nikauliza " Tukimwacha hai lazima kuna siku ataleta balaa huyu" akasema " Sasa nani atakuwa anatusaidia kazi hapa?" nikauliza " Nitamleta mdogo wangu yule aliyemaliza form four" akajibu " Aaah! Kama ni yule poa" nikasema " Poa? Sio poa kisa mzuri uje unigeuke? 
Nitakuua kwa mikono yangu" akasema kwa chuki Nilibaki nimejiinamia ila katika hali halisi alikuwa na haki ya kusema hivyo kwa sababu mdogo wake alikuwa mzuri mara sita zaidi yake na alikamilika kila idara. Tulilala kimya kila mmoja akitafakari la kwake,mimi kwa upande wangu nilikuwa najalibu kupiga picha juu ya mdogo wake na shemeji alivyokuwa mpaka usingizi ukanipitia Asubuhi tuliashwa na yule binti wa kazi kwa sababu kulikuwa na mgeni. Shemeji alirudi chumbani speed na kuniomba niwahi kutoka kwa sababu mama amefika " Mama atatufumania baby pz tafuta namna utoke humu chumbani" akasema

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.