PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE (28)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka na kutaka kukimbia ila shemeji akanishika mkono "Unakimbia nini?" aliuliza " Hapana sikimbii" nikamjibu " Basi kaa utulie" akasema " Unaham ya kufa kijana?" kile kichwa kikaongea Nilistuka tena na kutoka mbio na kwa bahati nzuri Shemeji alikuwa amejisahau hivyo nikamuacha amekaa pale pale Nilikimbia speed kali ajabu ambayo nahisi hata Usain bolt angetokea pale asingenishika kwani nilikuwa nakanyagia vidole vya miguu. 
Spee yangu haikunifikisha sehemu kwani mita mia mbili kutoka eneo lile nilishangaa kukuta nyoka mkubwa sana kalala njiani Nikageuza njia na kuelekea upande mwingine kwa speed kali zaidi ya ile ya kwanza ila sikufika mbali nikakuta mwili wa binadam ukiwa umelala bila kichwa. Nilichoka sana,nikasimama nikiwa nimepigwa na butwaa kwa muda ila akili iliponirudia nikageuza na kuelekea upande mwingine tena. 
Kwa wakati huo nilibaki nakimbia huku naangalia nyuma mpaka nilipojikuta nagongana na kitu kwa mbele Kugeuka nikakuta jamaa mmoja akiwa uchi wa mnyama ameanguka chini kutokana na kile kikumbo changu ila pembeni yake alikuwepo mwenza. Wale jamaa walikuwa wanafanana ajabu,na cha ajabu zaidi yule aliyeanguka aliposimama alikuwa na jicho moja na mguu mmoja kama mwenzake wakaanza kurukaruka huku wakija upande niliokuwepo,nilipogeuka nyuma ili niondoke nikashangaa kuona chini kile kichwa cha yule mganga " Kijana huwa sikimbiwi,,hahahahahahahahah!!hahahahahahaha!!!" kile kichwa kilitoa sauti na kumalizia kwa kucheka Nilijikuta nguvu zikiniishia pole pole na kisha
nikaanguka chini kama mzigo UPANDE WA DOKTA Tangu tunaondoka pale Dokta alihisi kuna hatari inayomsogelea hivyo akaanza kuandaa mipango ya kuuiba mwili wa kaka kisha atoloke nao kwenda nje ya nje " Mke wangu naomba uandae safari yangu ya ghafla nataka kwenda Afrika kusini" alimwambia mkewe kwenye simu " Kuna nini mme wangu? 
Na mbona mapema?" aliuliza mkewe " Utajua nikija" akajibu kifupi na kisha akakata simu Aliondoka na kwenda kuitisha kikao cha ghafla na madaktari wenzake ili awaeleze tatizo linalomkabili yule mgonjwa " Jaman,huyu mgonjwa wetu yuko hatari......" hakumalizia sentensi yake akakumbuka agizo la Shemeji " Mimi ni hatari zaidi ya unavyofikili,umekataa kufanya kazi yangu,nimekuacha hai kwa sababu maalum,kama una akili funga mdomo wako ila kama unajifanya jeuri fungua mdomo wako,tutakutana mbinguni" 
Alipokumbuka maneno ya Shemeji alijikuta akipata kigugumiizi " Nini Dokta? Haatari ip?" akauliza mmoja wa wale madaktari " Aaah! Hapana nilitaka kusema kuwa nahitaji kumsaidia huyu mgonjwa,hivyo nahitaji kuondoka naye kesho asubuh kwenda Afrika ya kusini kwa matibabu ila nataka hili swala libaki siri ya Hospital" akajibu Majadiliano yalichukua saa nzima kwa sababu wale madaktari walitaka kupewa sababu halisi ila baada ya majadiliano ya muda wakakubali kumruhusu Baada ya kupewa ruhusa ya kumsafirisha Kaka,Dokta alijiandaa na kisha akaondoka kuelekea nyumbani kwake Kitu ambacho Dokta hakujua ni kuwa alikuwa akifatiliwa nyendo zake zote na vijana wa shemeji Musa aliyekuwa kiongozi wa ule msafara aliwaacha vijana wake wamfatilie Dokta na kuhakikisha wanamteka na yeye akabaki hospitalin Alijitahid kwa mbinu zote akampata Daktari mmoja na kwa kutumia ushawishi wa pesa akafanikiwa kupata siri ya kaka kusafilishwa kisiri kuelekea Afrika kusini na yule Daktar " Alipanga kesho kumsafilisha jamaa kwenda Afrika kusini ili atibiwe....ndiyo.......muda si mrefu vijana watakuwa naye mkoni....ndiyo bos.....unahitaji tuondoke na huu mwili wa mme?......sasa hivi?.....sawa bos...umesomeka" aliongea kwenye simu Mussa na shemeji.

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.