PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA (27)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Nilishtuka sana kusikia kuwa shemeji alishawahi kuua na yeye akahisi kitu kwangu " Huyu mbona kashtuka? Ina maana dawa imeisha? Mtaalam alisema ikishika hatakuwa anajielewa ila huyu kujielewa huku anakutoa wapi?" aliwaza shemeji " Unataka kujua nilimuua nan?" akauliza shemeji " Mmmmmh! Eeeeeee! Aaaah! Hapana" nilishikwa na kigugumizi cha ghafla " Nikwambie kitu Junior?" akasema " Niambie shem" nikajibu " Tangu nizaliwe nilishawah kumpenda mwanamme mmoja peke yake! 
Unataka kumjua?" akasema " Ndiyo" nikajibu " Ni wewe hapo" akasema Muda huo wote nilikuwa nimechanganyikiwa na nilikuwa na hofu kubwa sana " Aaaa! Kwani kaka hukumpenda?" nikauliza " No siku mpenda,sikia nina historia mbaya sana niliyopitia katika maisha yangu,nyie wanaume ni watu wabaya sana na hamfai kuishi,nilishaua wanaume wengi sana na kaka yako ningeshamuua ila wema alionitendea ndo ulisababisha nimuache hai,nilikubali kuolewa naye kwa sababu aliamua kunisaidia,ila sikumpenda na bado nilipanga kuwaua wanaume ili kulipa kisasi changu tatizo lilianza nilipokuona wewe,nilikupenda na sijui hisia zilitoka wap? 
Ila nilikupenda na ninakupenda sana ndo sababu nikahangaika mpaka nikakupata sasa nikwambie kitu?" alieleza kiufup kisha akauliza na swali " eeeee? Yah! Nambie" nikaongea kiuoga " Siko tayali kukupoteza,niko tayali kuua watu elfu ila sio kukupoteza kwa sababu umeupa moyo wangu faraja na raha ambayo sikuwahi kuipata" akasema Nilibaki kumwangalia tu nikiwa sina cha kuongea " Kwani wanaume walikufanya nini shem?" nikamuuliza "

Walinipa mateso makubwa sana,wakausaliti moyo wangu kama ambavyo wewe unataka kufanya,sitaki kukuua Jun na nitalilinda penzi langu kwako"akasema Nilionesha mshtuko ambao ulimpa nafasi ya kutekeleza alichokipanga Alitoa bastola pale pale naa mimi nikabaki kupigwa na butwaa " Ee-aaa! Shem? Una bastola? Unaataka kuniua na mimi?" nikaongea kwa kiwewe " Nilikufanyia vitu flan ili twende sawa,umefanyaje vikatoka! 
Nijib au ufe sina masihara sasa" akfoka " Eeee? Unase.." sikumalizia nikapigwa kofi moja kali sana " Unajibu au haujib?" akauliza " Nitajib,,ni Dokta ndo amefanya hivi" nikaropoka " Ok,kumbe anayaweza?,sasa sikia endesha gari mpaka nitakapokwambia" akaniambia huku ameielekeza ile silaha kwangu Nilianza kuendesha gari huku nikiwa na uoga bado kwenye akili yangu nikifikiria cha kufanya ili niondokane na lile sakata. Shem alitoa simu na kupiga namba flani "
Eeee....Musa,,change the mission,,,,yap,,,,,naomba mmchukue yule Dokta akiwa mzima...yap namhitaji akiwa hai...kaingilia kazi...kazi njema" akamaliza na mimi nikafaham kuwa Dokta nimeshamweka hatarini Niliendesha gari akinielekeza njia za kupita mpaka tukatokea kwenye uwanja wa michezo wa Azam wa chamazi Tukaacha barabara ya lami na kupinda kushoto kwenye barabara ya vumbi Tulienda kwa umbali wa kama kilometa tatu tukashika pori dogo na kuingia " Paki gari hapa na nipe funguo" alitoa maagizo na nikayatekeleza 
Tuliongozana kuingia kwenye msitu flani kwa ndani sana. Tulitembea umbali mfupi na kutokeza kwenye kajumba kanyasi na makuti kalikochoka sana " Mtaalam......mtaalam.....nimekuja mkuu" aliita " Pita ndani nilishakuona" sauti ikatokea ndani Tukazama ndani na kukuta kichwa cha binadam kimekaa kwenye ungo chenyewe " Kaaeni hapo chini" kile kichwa kikaongea Nilishtuka kukutana na maajabu kama yale na kutaka kukimbia ila Shemeji akaniwahi na kunishika.

ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.