PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA (26)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Shemeji alifurah mno mpaka nikabaki namshangaa " Naona nikuulize kitu shem?" nikasema " Uliza ila sitak uniite shemeji tena,ita baby au mke wangu" akasema shemeji " Sawa baby,hivi ulishawahi kuua?" niliuliza lile swali maksudi kwa sababu jinsi shemeji alivyo handle lile swala ni kama mzoefu " Kwa nini umeniyuliza hilo swali?" akasema " Nimetaka kujua tu,samahan kama nimekukwaza" nikasema " Nitakujibu nikitoka hapa,samahan tusiongelee hilo swala hapa" akajibu Ikabidi nitulie na kusubir kitakachofatia.
Baada ya muda mfupi Dokta alirudi na barua mkononi kwake akatukabidhi " Mnapaswa kuandaa mazingira ya kumpeleka hivyo hospital imewapa siku mbili za maandalizi ili yakikamilika mje kumchukua mgonjwa wenu" akasema Dokta "No Dokta,siku mbili nyingi sana,sisi tunamtaka hata sasa" akajibu shemeji " Hapana,hatuwezi kuwapa mgonjwa kirahisi hivyo,lazima sheria zizingatiwe,nendeni nyumbani mkaandae mazingira kisha mtamchukua mgonjwa wenu kesho kutwa" akasema Dokta " 
Sawa ila natumaini kesho kutwa hamtatusumbua tena?" akauliza shemeji " Hatutawasumbua ila itanidi mfate taratibu zinazotakiwa ndo muuchukue mwili na pia hatutawapa mwili kirahisi,mtasindikizwa na gari ya wagonjwa na Daktar mmoja ambaye serikali imemtumia kuwasaidia mgonjwa akipata shida njian" akajibu Dokta Shemeji alichoka kabisa, " Daktari tena?" akauliza " Ndiyo,huyu mgonjwa katoka chumba mahtuti mnataka tuwape kirahisi rahisi? Akipata tatizo njian mtafanya nn? 

Dada sheria lazima zifatwe" akajibu Dokta kwa kujiamin " Poa"" Shemeji alisema kwa hasira kisha akanyenyuka na kutoka nje Baada ya shemeji kutoka nje yule Dokta alinipiga kofi moja la usoni nikajikuta nakuwa mwepesi sana nikahisi nimetua mzigo mkubwa sana " Acha ujinga, nimekusaidia baada ya kugundua umefungwa,ukiacha kuwa Daktari wa taaluma bibi yangu alinirithisha uganga wa kienyeji, nilipokuona kwenye rada zangu niligundua kuwa umetunzwa ndo maana unafata unachoambiwa,sasa nimekufungua,nenda na jifanye unamtii huyo mwanamke ila uje urudi nitakwambia cha kufanya,cha msingi usioneshe mabadiliko yoyote" alisema Dokta Me mwenyewe nilibaki najishangaa,nilijiona kama mjinga flani nikaanza kujiuliza kwenye akili yangu ninafanya nini? 
Nilitoka kwenye chumba cha Daktari baada ya yeye kunipa mawasiliano yake ili tujue namna ya kumsaidia kaka Niliingia kwenye gari na kumkuta shemeji amechanganyikiwa " Tunafanyaje sasa? Na hali inaanza kuwa ngumu?" nikauliza " Hapa inabidi huyuhuyu Dokta amuue kakako na hakuna jinsi" akajibu Shemeji " Si uliona amekataa unafikili tufanyeje ili akubali?" nikamuuliza Hakunijibu bali alichukua simu yake na kubofya namba flani kisha akasikiliza " Nipo ndani ya gari njoo" akakata simu Dakika chache baada ya shemeji kukata simu vipande vya njemba viliingia ndani ya gari na kukaa siti ya nyuma " Ndiyo bosi" wakasema " 
Kuna Daktari anayemhudumia yule marehemu,ana macho ya kengeza then anaongea kihaya,mfatilieni kisha mjue anapoishi na kila kitu chake nitawapa kazi ya kufanya leo hii hii" akasema " Ndiyo bosi" wakajibu " Kumbuka huwa sisamehi uzembe ila hii ni nafasi ya mwisho nimewapa,mkishindwa vichwa vyenu halali yangu,haya potea" akafoka Wakatoka na kutuacha peke yetu nikaona nimuulize mpango alionao " Nitamteka mke au mtoto wa huyu Dokta kisha nitamlazimisha kufanya kazi yangu" alinijibu " Hivi shem ulishawahi kuua kabla?" nikajikuta narudia swali langu " Ndiyo,tena sio mmoja" akajibu kwa kujiamin Nilihisi haja ndogo ikipita!!

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.