PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO (25)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Dokta alishtuka sana kutokana na maneno ya shemeji " Kwani yule sio mmeo?" aliuliza " Ni mme wangu ndiyo ila mimi ndo ninayetaka afe! Tuache mambo mengi Dokta nisaidie kwa hili na mimi niko tayali kufanya chchote" akasema Shemeji " Hapana dadangu,hili swala ni kinyume na maadili ya kazi,NO sitaweza" akasema Dokta " Nitakupa milion mbili" akasema Shem " Siwezi" akajibu dokta " Milioni tano" akasema shemeji " Sikia,uliza mtu yeyote yule Dokta Rweyemamu ni nani? Nina pesa na ninaijua taaluma yangu vizur,siwez kuchukua hata million mia moja ni visent tu hivyo" akajibu kwa malingo ya kihaya ndani yake " 
Mara ya mwisho million kumi" akasema shemeji tena kwa msisitizo " Huelew kiswahili ee? Naomba niondoke kama ho upuuzi ndo umeniitia" akasema Dokta " Sikia Dokta,yule mwanamme atakufa tu hata wewe usihusike,tena kwa mkono wangu hivyo ni bora uchukue hii pesa ikusaidie kwa sababu usipoichukua ataichukua mwingine na atafanya kazi" akaongea kwa malingo shemeji Yule Daktari alimwangalia shemeji kwa jicho la mshangao sana " Hivi wewe ni binadam wa kawaida kweli? 
Unafikilia kumuua binadam mwenzako kama kuku? Aisee wewe ni gaidi na si binadam" akasema Dokta kisha akaamka na kuanza kuondoka 
" Sikia Dokta" akasema Shemeji na Dokta akasimama kusikiliza " Mimi ni zaidi ya unavyonifikilia,sasa umekataa pesa yangu basi nakupa onyo,fungua mdomo wako tu na kifo kiwe halali yako,sirudii kukupa hilo inyo ila utakutana na utekelezwaji pekee,na pia yeyote atakayetaka kuifanya hii kazi usimuingilie kwa namna yeyote,kwa heri" aliongea huku tukimpita Dokta na kuondoka.

Dokta alibaki mdomo wazi akituangalia wakat tukiingia kwenye gari na kuondoka,naamin alimshangaa sana Shemeji. Tulipofika nyumbani hakuna aliyekuwa na ham na mwenzake, hata bafuni kila mmoja aliingia kwa muda wake mwenyewe kisha tukakutana chumbani " Tunafanyaje sasa? Na hili swala limeanza kujulikana kwa watu wengi?" nikamuuliza shemeji " Tulia hii movie nimeiandika mimi,na ninaicheza mimi,stelling hauawi,lala kesho nitakuonesha cha kufanya"akasema shemeji 
Kweli kila mmoja akaingia kulala tena mzungu wa nne kwa sababu kwa hali aliyokuwa nayo shemeji alikuwa sio wa kuongelesha kwani hata mimi nilimuogopa kuwa anaweza kunipiga Asubuh tuliamka kama tulivyolala,kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani Baada ya kupata kifungua kinywa tuliondoka kwa pamoja kuelekea Hospitalinu,njian shemeji alipiga simu " Mmeshindwa kufanya kazi ya kwanza,sasa nawapa ya pili,mkishindwa subirieni vifo vyenu,,nawaomba hapa Muhimbili" alimaliza kuongea n kukata simu
 Hata mimi nikajikuta naanza kumuogopa shemeji. Tulifika Muhimbili na kuingia kumuona Dokta anayehusika na mgonjwa " Dada sihitaji kuingia kwenye ugomvi na wewe ikizingatiwa sikujui na wewe hunijui" akasema yule Daktar " Kwa hiyo? Unatakaje?" Shemeji akamuuliza kibabe " Nimefikilia sana juu ya ombi lako,ukweli siwezi kulifanya na siwez kuua kwa sababu ni dhambi,nilichofanya ni kumuandikia mgonjwa wako ruhusa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi na si hapa nchini,na wewe utajua huko huko cha kufanya" akasema Dokta Nikashangaa kuona Shemeji akitabasam 
" Kazi nzuri,sema unataka kiasi gan kikupozee koo" akasema shemeji " Hapan,sihitaji chochote kile" akajibu yle Dokta Aliinama na kuchukua karatasi flani kisha akatoka nikabaki na shemeji " Kazi imeisha,hakuna kupelekwa nje ya nchi wala nin,tunaenda kumuulia nyumbani,au vip mpenzi?" aliongea ila neno mpenzi nilihisi kama kanitukana,nilijisikia vibaya sana.

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.