PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE (24)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Baada ya shemeji kusema kaka hajafariki nilishtuka sana mpaka pombe zote zikaniisha kichwani " But how? Kivip? Kinehe? No imposible" nilijikuta nachanganya lugha tatu kwa mpigo kwa hamaki Sehemji hakunijibu kitu,alichukua ile simu yake na kunikabidhi kisha akakaa kitandani huku kachoka balaa Nikaichukua ile simu kwa papara kisha nikafungua sehemu ya ujumbe na kuusoma
 " Shemeji mmeo kapata ajali mbaya ya gari,amelazwa hapa Mihimbili ingawa hali yake sio mbaya sana ila tumekutafuta hupatikani,ukipata ujumbe huu tuambie uko wap na njoo haraka" ile message ilisomeka hivyo Na mimi nikachoka kabisa,hajafa?!! Na hali yake sio mbaya?" nikajikuta nikiongea kwa sauti Shemeji alionekana kukata tamaa kabisa,aliichukua ile simu kisha akapiga no flani
 " Nyie wangese kwa nini mmenidanganya?.....mnaona pesa yangu ya kuchezea?......sasa kwa taarifa yenu mimi ni gaidi mara kumi zaidi yenu.....sittaki kusikia maelezo kwa sababu mtu ni mzima.....rudisha pesa kesho asubuh" alimaliza kuongea kisha akakata simu " Vip? Wanasemaje?" nikamuuliza " Wapuuzi sana hawa,unafikiri wana cha kusema? Hapa kitumbua kimeingia mchanga tukaoge" akasema shemeji Kwa kipindi hicho kulikuwa hakuna mapenzi tena,zile swaga za kubebana kwenda bafuni na kuogeshana hazikuwepo kabisa.
Tuliingia bafuni kwa pamoja huku kila mmoja akiwaza ya kwake,tukaoga fasta kisha tukarudi chumbani na kuvaa nguo haraka. Safari yetu ilianza kuelekea Hospital ya Rufaa Muhimbili kwa ajili ya kumuona mgonjwa. " Shem tulikuwa nje ya mji kibiashara,samahan sana tuko njiani tunakuja,tumeshaingia Dar" alisema sehemeji kwenye simu akiongea na rafiki yake kaka mkubwa kibiashara Tulipofika tulimkuta shemeji akiwa chumba cha wagonjwa mahtuti akitibiwa hivyo hatukupewa nafasi ya kumuona.

" Mgonjwa wenu ana hali mbaya sana,amevunjika miguu yote,na pia sehemu kubwa ya kichwa imepasuka na baadhi ya viungo vyake vimevunjika kabisa hivyo tunaomba mtupe muda wa kumshughulika" alisema Daktari " Samahan Dokta nina mazungumzo na wewe nje ya ofisi naomba ukiwa off tu unitaarifu tuonane kuna swala la msingi la kujadiliana kuhusu huyu mme wangu" alisema Shemeji akimkabidhi yule Dokta bussines card yake Dokta aliichukua kisha sisi tukaondoka na kwenda kwenye gari ikiwa kama saa moja za usiku " Tunafanyaje shem? Coz naona maji yamefika shingoni" nikauliza 
" Kaa utulie mimi ndo stelling,naendesha picha nzima,,,Junio nataka uniahidi kuwa huyu bwana akiondoka utanipenda kwa dhati,hutanisaliti wala kunizunguka kwa namna yeyote" akasema shemeji " Nakuahidi shemeji kwani una wasiwasi na mimi?" nikajibu na kumswalisha " Sijasema nina wasiwasi na wewe ila nakupa tahadhari,nafikiri umeshaona watu ninao shilikiana nap na ugaidi wangu ulivyo,kwa taarifa yako wale vijana kesho nawatanguliza kwa sir god,sasa sitaki mchezo na kaa ujue siku ukinigeuka tu,utakuwa umeshajitangazia kifo" akasema Maneno ya shemeji yaliniogopesha sana ila nikajikaza kiume.
 Tuliondoka na kwenda kukaa bar iliyokuwa kalibu na ile Hospital tukisubir yule dokta atoke kazini Saa tatu yule Dokta aliwasiliana na shemeji na akaelekezwa tulipo kisha akaja " Najua mmeumia sana,poleni sana niwaahidi tu kuwa kwa juhudi zangu mme wako atapona na kuwa mzima kama zaman" aliongea maneno ya kutuvutia ili tumpe chochote amsaidie kaka " Dokta mimi sitaki mme wangu apone,nimekuita hapa ili tusaidiane kama ndugu,nataka yule bwana afie pale pale ndani" aksema shemeji Dokta alishikwa na mshangao!!!!!

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.