PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA AROBAINI NA NANE (48)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu." Shemeji ni jambo gani hilo unalotaka kuongea na mimi na hutaki dada ajue?" akauliza Joan " Kwanza niahid kuwa wewe ni mtu mzima na hata kama litakuudhi kiwango kikubwa hayatafika kwa dada yako?" nikamwambia " Hilo jambo basi sio jema maana kama unahidi linaweza niudhi mpaka kumwambia dada mmmmh! Akasema " Basi shem yaishe! Vip umepika?" nikabadilisha mada " Sitak!
 Unabadilisha maada ya nini? Sema ulichotaka kusema" akasema " Sa nitasemaje ilihali wewe umeshaanza kunitisha? 
Unataka unipe kesi bure?" nikamwambia " Amna bana me ni mtu mzima,nina akili zangu timamu na wala sihitaji kusema au kuongea na mtu juu ya mambo yangu,nina maamuzi yangu mwenyewe,jiamin na niambie tafadhali" akasema " Kweli?" nikauliza " Ndiyo sema tafadhali" akajibu " Hivi unaonaje? Navyoishi na dada yako?" nikamuuliza " 
Mbona kawaida kama mke na mme huku mkipendana kwa dhati" akajibu kwa style niliyosoma kama kunikwepa " Hivi wewe unakubaliana na tamaduni za kurithi?" nikamuuliza " Kiukweli nimeshangaa sana! Hivi ungekuta kakako alikuwa mwathilika na dada ungefanyaje lakin? 
Na wewe kwa nini ulikubali?" akauliza " Shem hili ni shinikizo jaman,mimi sijapenda na sifurahii hata kidogo,natafuta namna ya kutoka humu" nikajibu " Heeee! Kwa hiyo humpendi dadangu?" akauliza kwa mshangao " Ndiyo tena simpendi kabisaaaa" nikajibu " Jaman! Mbona huwa nikiwaona pamoja naona mahaba teele? Au unazuga? Na kwanini usimwambie?" akauliza " 

Dadako ni katili tofauti na unavyomfaham,namuogopa kwa kweli,na ninashangaa imekuwaje anipende kama alivuokuwa kwa kaka na hata siku ya kumbiwa kurithiwa hakukataa ila me simpen" nikajibu " Mmmmh! Una mtihani? Sasa wewe unampenda nani kama dada humpendi na unaishi naye?"akauliza " Mimi nakupenda wewe" nikamjibu " Mmmmh! " akaguna " Usishangae Joan ni kweli nakupenda tena nakupenda kwa dhati,tafadhali kuwa wangu" nikamwambia "
 Yaan shem unanichanganyia tu habari,unaishi na dadangu af mimi umeniona jana tu leo unanipenda huoni huo ni uongo wa wazi kabisa? Hapa unanitaman tu na unataka kunigombanisha na dada" akalalamika " Hapana Joan,mimi sijawahi kumpenda dada yako kabisa! Ila naomba utambue jambo moja la msingi kwenye neno kupenda,kupenda ni hisia na sio maneno,hisia huwa haziji kwa mwaka mzima au mwezi! 
Hapana,hata mtu unayekaa naye mwezi mzim bila kumpenda siku hisia zikija utajikuta tu! Kwa sababu hiyo hisia zinatokea ndani ya sekunde kadhaa ndipo moyo unapopewa taarifa ya kupenda,kama hisia hutokea kwa sekunde kadhaa basi hata mtu uliyemuona kwa mara ile ya kwanza unamuona hisia zikifanya kazi yake basi dakika hiyo hiyo na wewe utajikuta unampenda" nikamwaga sera " 
Kwa hiyo wewe unataka kuniambia hisia zilikushika jana au leo?" akauliza " Zimenishika jana ghafla baada ya kukuona na hapohapo taarifa ikapita kwenye ubongo mpaka kwenye moyo kuwa huyu ndiye chaguo langu,kwani una mtu?" nikamwaga tena sera " Me sina mtu shem lakin si sababu ya kuwa na wewe af kwani umenipendea nini shem? Na dada ananizid uzur?" akauliza kimadeko " Kwanza naomba ufute kauli,dada yako hakuzidi uzuri,wewe ni mzuri sana tena zaidi ya sana,angalia umbo lako linavyopendezea kila nguo unayoivaa, limegawanyika kiafrica zaidi utadhan Cleopatraza misri,pili angalia sura yako ya upole inavyovutia kuangalia kila saa, na kwa weupe wako huu sidhani kama kuna haja ya taa,angalia kiuno chako kilivyomegeka na kutengeza hipsi nzuri na zenye mvuto kwa kila mtu kuangali,,angalia mguu wak......." sikumaliza 
Ghafla kabla sijamaliza kumlainisha na sifa tukasikia kengele ya getini ikilia Nikaogopa mpaka nikahisi jasho jembamba likinitoka!!!

ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.