PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA AROBAINI NA TATU (43)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mama alishtuka sana kusikia shemeji anasema kuwa yeye ndiye anayepaswa kufata kwa wanaotakiwa kufa " mamangu,ni kipi kibaya nilichokifanya mpaka ufikie huko?"akasema mama kwa hofu kubwa "tatizo lako una kiherehere na unapenda kuingilia mambo yasiyo kuhusu"akajibu shemeji "lakin mamangu? kulikuwa na tatizo gani mpaka ukaamua kumuua mwanangu na bado unaendelea kuua? kwa nini usibadilike?"mama akaendelea kumuulia shemeji "matatizo ni mengi,sasa sijui unataka nikueleze lip? la mwanao? au kwa nini naua?"
akauliza shemeji "kwanini unaua?akasema mama "hilo ni vigumu sana kukueleza kwa sasa,kwa sababu ni historia ndefu sana ila mimi nitakwleza kwa nini nilimuua mwanao"akasema shmeji "haya kwa nini ulimuua mwanangu? na kwa nini unataka kuniua na mimi?"akauliza mama
 "labda nikuulize wewe mimi na mwanao tulikuwa na miaka mingap kwnye ndoa bila mtoto?"akauliza "mitatu"akajibu mama 'na unajua kwa nini?" akauliza shemeji "hapana sijui,mimi nilidhani ni uzungu wenu wa kupanga uzazi?"akasema mama "hakuna uzungu hpo mama! mwanao alikuwa hana uwezo wa kunipa mtoto"aksema kwa kujiamin sana "heeeeee!!!!! unasem kweli mwanangu?"akauliza kwa hamaki mama 

"ndiyo,mwanao alikuwa tasa,nilivumilia hilo swala kwa muda mrefu sana ila nikafikia hatua nikashindwa,na mimi kama mwanamke yeyote yule napaswa kupata mtu wa kuniita mama, nilishafikilia kuachana na mwanao ila alipotokea huyu Junior nikaona haina maana ni bora kama ni mali zibaki katika mikono yenu na kama ni dam niipate kutoka katika familia hii hii badala ya kwenda nje,sasa nilifanya makosa?"
akaeleza kirefu sana shemeji Mama aliinama chini machozi yakamtoka,alikuwa akilia hakika na alikuwa dilema ya kukubaliana na uamuzi wa shemeji au kuuukataa "lakini hukutakiwa kumuua"akasema mama "ilikuwa lazima nimuue kwa sababu bila kumuua msingenielewa na nisingepata nafasi ya kuishi na Junior mama"akalalamika shemeji "nipeni nafasi nitafakari hili jambo ni zito sana jaman,nikiwa sawa nitakuja na majibu muafaka"akasem mama "haya mama,ila kuwa makini sana"akasema shemeji "sawa"akajibu mama 
Baada ya mama kuondoka shemeji aliinama kwa muda kisha akanyenyuka na kuniangalia "itabid mama atupishe"akasema "una maana gani kuwa atupishe?"nikauliza "mama akiendelea kuwepo kitakuwa kikwazo kikubwa sana kwetu"akasema "kwa hiyo unataka kumuua mama? siko tayali"nikajibu "hivi unakumbukumbu nzuri kuwa wewe ndiye uliyemuua kakako? na hii kesi ikifumuka mtuhumiwa ni wewe na si mimi?akasema shemeji Nilishtuka baada ya kugundua kuwa huo ndo ukweli wenyewe "kwa sababu hiyo,ukikamatwa ina maana na mimi nitakamatwa kwa mauaji ya dokta na yale ya wzee na mimi sipo tayali"akasema 'tafuta njia nyingine ila sio kumuua mamangu'nikasema kwa kujiamin "sasa sikia,kwa ajili ya uhai wangu,kuna option mbili aondoke mamako au muondoke wote jiandae kwa hilo pia'akasema kwa kujiamin Nilishtuka sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.