PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA (41)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Nilishtuka kusikia kuna mauaji yamefanyika pale msibani tena mchana kweupe " Mmmh! Shemeji ameshaanza au? Na hawa nao wamemkosea nini tena?" nilijiuliza Nilitulia ndani ili watu wasije shtukia kinachoendelea kwangu kuwa sikuwa nimezimia bali niliigiza Kelele kule nje zilizidi kuwa nyingi sana,wakina mama walilia sana kila mmoja akawa anaongea la kwake " Jaman kuna nini kinaendelea hapa? 
Iweje hawa wafe kirahisi hivyo?" watu waliendelea kusemezana Wakati nimekaa na wale jamaa pale ndani nilishangaa kumuona shemeji anaingia " Vip shem mmeshazika tayali?" nikamuuliza " Ndiyo shem wangu,jaman samahani,naomba mnipe nafasi kidogo niongee na shemeji yangu hapa" aliongea kiupole 
Katika hali halisi ya kawaida ya kimaisha Shemeji alionekana binti mmoja mpole na mcheshi,asiye na makuu kabisa,hata pale msibani nilisikia watu wengi wakimsifia " Jaman mdada wa watu mpole na hana makuu kabisa! Leo anabaki mjane" watu wengi walikuwa wanamuongelea vizur " Shem kuna nini kinaendelea?" nikaongea kwa sauti ya chini sana " Nishukuru mimi bwege wewe! 
Af unavunga kuniona sifai,ungeshakufa mpaka sasa" akasema " Kwanini shem? Kuna nini kinaendelea?" nikauliza kwa mshangao " Sikia Jun,mimi ni tofaut na unavyofikilia,nafanya mambo yangu kwa utaratibu,wewe nimekutegeshea kifaa cha mawasiliano tangu msiba ulivyoanza,hiyo yote ni kuwa makini nisije nikafanya kosa lolote lile" akasema " Mmmh! Cha nini sasa? Unafikiri naweza kukusaliti" nikamuuliza " 

Sio kunisaliti,hasa hasa ni ulinzi wako,pia kila sehemu nayoenda lazima vijana wangu wawepo na wafatilie nyendo zote mbaya zinazonihusu" akasema " Sawa sasa hao wazee uliowaua wanahusika vip?" nikaendelea kuuliza " Wakati unaongea na mama kuhusu swala la kutokwenda makaburin kwa sababu ya mila zenu nilikuwa nawasikiliza lakini pia vijana wangu walikuwa wanafatilia nyendo za watu wote wanaoonesha shaka juu yangu au wewe" akasema " 
Nini kikaendelea?" nikamsaili " Wakati nyie mnaongea wale wazee walishawashtukia tayali hivyo walikuja na kusikiliza kila mlichokuwa mnapanga na vijana wangu walikuwa wanawaona vizuri" akasema Nilishtuka sana kusikia kuwa mipango yetu ilikuwa imeshajulikana " Ndo maana nilipozimia nilisikia wazee flani wakisema nadanganya?" nikauliza kwa mshangao " Sio kuzimia,sema kuigiza kuzimia" akanisahihisha " Aya ndelea basi ikawaje?" nikamwambia " 
Wale wazee walifatiliwa na vijana wangu na wakasikiwa wakipanga kukuumbua ukicheza huo mchezo na pia kukulazimisha wewe kwenda makaburini ili ufe au kuumbuka,nilipoona hivyo nikajua kuwa ukiumbuka wewe na mimi nipo hatarini" akasema " Mama yangu" nikabaki kushangaa " Vijana wangu wakatafuta upenyo wa kuwaondoa wale wazee,ila wakawa wanajichanganya na watu ikawa ngumu, ila wakati wale wazee wanakuja kukuumbua watu waliwafukuza na wao wakeelekea kule migombani na kupanga mbinu mpya za kukuumbua na huko huko ndipo vijana wangu wakawamaliza" akamaliza kusimulia " Duuuu! Kweli leo ningepatikana,lakini kwa nini wamewaua sasa? 
Wasingeweza kuwateka mpaka muda wa mazishi uishe?" nikauliza " walileta ubishi kwa sababu vijana walitaka kuondoka nao,na pia tungewaacha baadae wangeleta madhra" akasema " Sasa sikia, jitahid kuwa makini kwa kila unachokifanya" akasema na kunyenyuka kisha akaondoka Nilitulia pale ndani nikiwaza ule uwezo wa shemeji nikahisi kumuogopa Wakati nikiwa bado mawazoni nikasikia gari za polisi zikipaki pale nje Majadiliano yalifanyika kwa muda pale nje na ghafla mlango wa chumba nilicholala ukasukumwa na wakaingia ndani askari wawili " Habari kijana?" wakanisalimia " nzuri shikamoo" nilijikuta nimewaamkia kwa sababu ya uoga " Tunakuhitaji kituoni tafadhali amka twende" wakasema Nilihisi haja ndogo ikipita!!!

ITAENDELEA ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.