PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI (42)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu." Kijana vip? Mbona unatetemeka hivyo? Hujiamin?" akasema mmoja wa wale askari " Ana haki ya kutetemeka kwa sababu ni kitu kigeni na cha kuogofya kwake" akasema shemeji ambaye hata sijui alipotokea " We ni nani unayemuongelea?" akauliza mmoja wa wale askar " Mimi ni shemeji yake,mimi ndiye mfiwa" akajibu kwa kujiamin " Okey mfiwa,tupo hapa tunamchukua huyu shemeji yako kwa mahojiano maalum" akajibu yule askar " Nipatieni kibali cha ruhusa ya kumkatama shemeji yangu" akasema kwa kujiamin Wale askar wakatazamana kisha wakajibu " 
Aaah! Unajua imetokea tu ghafla baada ya kupata maelezo kuwa vifo vya hawa watu vina uhusiano na huyu shemeji yako ndiyo tukaona tuende naye" wakajibu kwa kutokujiamin " Ni sheria ya wapi inayosema kuwa mtu anapelekwa polisi kwa kukamatwa bila kibali na pili akiwa mgonjwa! Ina maana hamuoni hali yake?" alikuwa anaongea kwa kujiamin sana mpaka nikashangaa " wee! Usitufundishe kazi sawa? 
Hapa nyamaza na huyu tunaondoka naye" akafoka mmoja wa askari " Nyie mnanijua vizur? Au mnanisikia? Chezeni na watu wengine na sio mimi hapa hatoki mtu,hamuwezi kuja kunivurugia msiba na kumchuka mfiwa,kama akili zenu zinafanya kazi hao wamepata matatizo huyu akiwa hana faham sasa mnamkamata kivip?" akafoka shemeji " Sasa unatufokea Mura?" akajibu askar mmoja mwenye lafudhi ya kikurya " Ndiyo nawafokea kwa sababu hamjui kutimiza majukumu yenu,,,,hebu subir" akasema kisha akatoa simu mfukoni na kupiga " 

Hellow......ndiyo advocate wangu,,,,,yah! Sasa fanya hivi,chukua ndege dakika ishilini uwe Moshi kuna watu wanataka kuniharibia msiba....ndiyo,,,wanataka kumkatamata dogo wakati hata kibali cha kumkamata hawana na pia hawana kosa la kumkamatia...ndiyo...make it faster" aliongea na simu kisha akakata ila kila mmoja alikuwa kaelewa aliongea na nan? " Sikieni kama mnajiamin na mna kiburi basi mchukueni huyo hapo muondoke naye na kisha tutajua pa kukutania" akasema wale askari waliangaliana kwa muda kisha taratibu wakapanda gari wakiwa na ile miili ya marehemu wale na kuondoka " 
Tunaenda ila nakuhakikishia tutarui hapa,kama kuna kitu kinaendelea mtajua tu" wakasema kabla ya kuondoka Walipoondoka Shemeji alimuita mama na mimi kisha tukakaa kikao cha siri na kipindi hicho tetesi mbaya zilishaanza kuzagaa eneo lile kunihusu mimi kuhusishwa na kifo cha Urio na Mushi " Mama usiwe na wasi wasi shemeji hatakamatwa kabisa" akasema shemeji " Sawa" akasema mama kiuoga " Subiri kidogo" akasema kisha akatoa tena simu " 
Hellow....unaonaje kwanza nikiwa siliana na Boaz hata nisaidia?....yah.......ok nipe dakika tano" akasema na kukata Shemeji alipekua simu kisha akapiga " Hellow...naongea na mkuu wa polisi mkoa kikanda wa kinondoni kamanda Boaz?....ndiyo....ni mimi Lilian bana mke wa marehem....ndiyo .....fanya kwa ajili ya upendo wangu kwako..kuna inshu hapa Moshi zinataka kuhalibu mambo naomba uwasiliane na mkuu wao haya mambo yasiende sehemu...ndiyo..nitatimiza unachotaka usijal baby...kwaher" akakata Kila mmoja pale alishtuka kuona shemeji anamuita Kamanda Boaz baby?!!!! Ila tukafanyia kichwani " Mnawaza nini sasa? Mnashangaa mimi kumuita baby?" akauliza " Hapana wala hatushangai" akajibu mama " Sikia wewe mama,unajua wewe ni mnafiki" akafoka shemeji " Kivip mwanangu?" akauliza mama " Ule mchezo uliokuwa unaucheza na Junior unajua ulishtukiwa na wale wazee? Na walipanga kuwaumbua na kumlazimisha Junior ajitokeze makaburini? Isingekuwa mimi kuwa makini unajua mngeshapotea? Nimeua kumlinda Junior,nitatembea na huyo Kamanda ili kumlinda Junior na kila nachofanya kwa sasa ni kwa ajili yenu na sio mimi Sasa angalia sana kwa sababu anayefatia kufa utakuwa wewe"akamalizia Mama alishtuka kidogo aanguke chini!!!!...

ITAENDELEA IJUMAA
Post a Comment
Powered by Blogger.