PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA AROBAINI (40)


Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Baada ya kumaliza kuongea na mama nilirudi sehemu waliyokuwa wamekuwa wamekaa wale vijana niliokuwa nao mwanzoni na kuendelea kusogoa " Sema nini chali angu? Yaan chukulia easy tu mwanangu? Af komaa kwa sababu hapa umebaki peke yako mtoto wa kiume au sio?" akasema mmoja wao " Yaan umene?..umenena chal angu,unajua arifu mother ako kwa sasa aanakutazamia wewe kama muhimili wa familia yenu hivyo unapaswa kuwa str...strong man " akasema mwingine " 
Af mwanangu dah! Sema pole sana ndo ya dunia" akasema mwingine Nikainama chini kwa majonzi,kisha nikanyenyuka huku machozi yakianza kunitoka " Ahsante sana jamaa zangu,,ila imen-i-uma s-a-na.." nikajitengenezea mazingira ya kulia na kweli ndani ya muda mfupi nikawa nalia sana Niliamua kucheza kabisa nafasi ya uigizaji ili kuyanusuru maisha yangu kama mama alivyosema Nililia huku washkaji wakinibembeleza pale na watu wazima wakaanza kushtukia kuwa kuna kitu kinaendelea pale 
Ghafla nikabadilisha pigo langu na kuanza kuhema kwa shida sana Hiyo yote ilikuwa mbinu yangu ili nipone kwenda kwenye makaburi kuzika " Jaman hamuoni huyu kijana anakosa hewa ndo maana anapumua kwa shida? Sogeeni pembeni na mmwachie nafasi ya kutosha" akafoka mzee mmoja " Kuna nini tena hapa?" akasema mmama mmoja aliyetokea pale pia " Aah! Sijui hawa vijana wamemfanyaje mwenzano ghafla akaanza kulia huku pumzi inamuishia kama unavyomuona" akajibu yule mzee " 

Sisi hatujamfanya kitu babu,tulikuwa tunamfariji hapa ili asijisikie mpweke" akasema mmoja wa wale vijana niliokuwa nao pale Nilipoona najaza watu nikaamua kurusha pigo la mwisho ambalo niliamin litamaliiza mchezo mzima Nilipumua kama mara tatu kwa nguvu na kwa kuvuta sana pumzi kama inanikosa kisha nikajiachia na kulegea kama mlenda! Kazi ikawa imeisha " 
Kijana,,,,,kija,,,,,kijana,,,,,aya aisee jombaa huyu kesha tangulia tena kwa mw....kwa mwana wa maria chalii" akasema kijana mmoja pale Ikawa hekaheka pale kila mtu akawa anahangaika kuyanusuru maisha yangu Mzee mmoja akaniinamia na kusikiliza mapigo yangu kwa muda kisha akanyenyuka
 Alichokiongea ndicho kilichofanya niamin binadam ni wanafiki na ndo maana mtoto anaweza zaliwa leo ukashangaa wanasema anafanana na mtu " Jaman bado anapumua ila anapumua kwa mbali sana tena sana,kuweni makin na ongezen kumpepea ili asije akatutoka" akase0a yule mzee " Jaman kuna nini hapa?" nikasikia saut ya mzee mmoja " Aah! 
Hapa huyu kijana amepatwa na majonzi ndo unaona hali imebadilika,yaan hapa tukicheza tunampoteza" akajibiwa " Si nilikwambia? Mchezo umeanza" yule mzee akasema huku nikisikia " Dah! Kweli aisee,wanaweza kuigiza ee?" akajibu mwenzake " Kabisa,jaman huyu hajazimia kabisa" akaropoka yule mzee " Wee mzee zinakutosha? Hajazimia nani? Unatuchuria ee? 
Tunaomba uondoke hapa yasije yakakukuta makubwa" akafokewa na mzee mmoja wapo " Jaman mwenzangu anachowaambia ni kweli kabisa,huu ni mchezo hapa hakuna cha kuzimia wala nini,huyu kijana na mama ya......" hakumalizia kuongea yule mzee watu wakamshambulia kwa maneno makali sana 
Walitukanwa na kufukuzwa eneo lile kwa hasira na watu,nilitaka kufa kwa presha pale chini baada ya wale jamaa kutaka kuhalibu mchezo,sikujua ni akina nani mpaka baadae sana Wazee kadhaa waliwaamrisha wale vijana wanibeba kisha waakanipeleka ndani kwenye chumba chenye hewa ya kutosha kisha feni ikawashwa " 
Kaeni naye humu wakati tukijiandaa kwenda mazikon,akiwa sawa mtatushtua na akizidiwa tuambieni tumuwahishe hospitalin" akatoa maagizo Nilitulia vile vile kwa zaidi ya masaa mawili ndipo nikaanza kuchezesha vidole vya mkono na taratibu nikajifanya kuwa fahamu zinanirudia Wakati narudisha fahamu kule nje zilisikika kelele nyingi ambazo ziliashilia tukio lisilo la kawaida
 " Oyaa kuna nini?" wale vijana wakaulizana " Unauliza kuna nini wakati tuko wote humu chali? Mbona una dharau hivyo" akafoka mwenzake Yule aliyeuliza hakutaka makuu alinyenyuka na kwenda huko nje baada ya dakika tano akarudi na jibu " Oyaa kuna watu ni kat?...katili chali angu!" akasema " Kuna nini jombaa?" akauliza mwenzake " Wale wazee waliokuwa wanaleta mdomo pale kwa chali yetu kuwa hajazimia! Cha angu wamekutwa hapo shambani wamekatwa vichwa ujue" akasema " Yesu na mariia yeleeeeuiiiiiiiii" akasema mmoja wao Nilishtuka sana!!!!!!

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.