NDANDA KOSOVO KUZIKWA SIKU YA JUMATANO DAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Baadhi ya wasanii pamoja na ndugu wa aliyekuwa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini marehemu Ndanda Kosovowakiwa katika msiba wa mwanamuzi huyo Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto waliokaa ni mjomba wa marehemu, Kardinal Gentle. (Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Na Francis Dande
Aliyekuwa Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini marehemu Ndanda Kosovo 'Kichaa' anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa mjomba wa marehenu Kardinal Gentle Ndanda Kosovo aliyefariki Jumamosi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema kuwa "licha ya familia kutaka marehemu kuzikwa Congo lakini wameshindwa kufanya hivyo kwa kuwa marehemu Ndanda Kosovo wakati wa uhai wake aliacha wosia wa kutaka kuzikwa Tanzania hivyo nimewajulisha ndugu waliokuwa Congo kuhusu jambo hili na wamekubali mwili wa marehemu kuzikwa hapa na sasa tunasubiri familia yake akiwemo mama yake kufika Tanzania ili kukamilisha taratibu za mazishi"

Kardinal Gentle ameongeza kuwa kabla ya kifo chake marehemu Ndanda Kosovo alikuwa anamiliki bendi iliyokuwa ikijulikana kwa jina la watoto wa Tembo.

Kardinal Gentle ameongeza kuwa merehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo na alilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.
Post a Comment
Powered by Blogger.