LEO KATIKA HISTORIA: JE UNAJUA KWAMBA RAIS MSTAAFU MH. JAKAYA KIKWETE AMETOKA FAMILIA YA WANASIASA? BASI SOMA HAPA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Jakaya Mrisho Kikwete tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015 alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.
Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.

Alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971).Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi, Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yakemwaka 1975.
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.

Mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho.
Kupanda ngazi katika siasa
Rais mtaafu mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na wilaya za Nachingwea na Masasi.

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.

Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.
Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.
Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.
Post a Comment
Powered by Blogger.