LEO KATIKA HISTORIA: HII NDIO HISTORIA YA MAREHEMU NDANDA KOSOVO YA KIMZIKI NCHINI TANZANIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ndanda alianza safari yake ya muziki akiwa nyumbani kwao Kongo ambapo baada ya kutua nchini alitamba na Bendi ya FM Academia International iliyokuwa maarufu baada ya kutoa Wimbo wa Wajelajela. Katika wimbo huo Ndanda alishirikiana na wasanii wakali ambao ni pamoja na Nyoshi El-Sadaat, Maluu Stonch, Mulemule FBI, King Blaize, Patcho Mwamba, Gento na wengine wengi waliuimba baada ya kutoka jela walikokuwa wameshikiliwa kwa ishu za kutokuwa na vibali vya kuwaruhusu kuishi na kufanya kazi Bongo.
Ndanda Kossovo alitoa wimbo mwingine akiwa FM Academia kipindi hicho alitamba na kibao "Chozi la Mnyonge" kabla mafahali wawili "Nyoshi El Sadat" na Ndanda Kossovo kutofautiana na kila mmoja akaanzisha kundi lake. Nyoshi akabaki na FM Academia "Wajelajela Gwaa" na Ndanda Kossovo akaenda kuanzisha Stono Musica "Wajelajela Original"
Ndanda aliondoka na wanamuziki mahiri kama Patcho Mwamba (huyu tunayemuona kwenye Bongo Movie), Maluu Stonch, Chai Jaba na wengineo. Baada ya kuunda Stono Muzika wakatoa kibao maarufu cha "Bibadamu" kilichokua na kibwagizo "sasa wanaanza kulia eeh Nuhu.. Eeeh Nuhu utufungulie safina.." Baadae wakatoa kibao "Jimmy Chocolate" ambacho kilivuma sana na kibwagizo cha wimbo huo kikawa kinatumika kama "soundtrack" ya igizo la Kidedea lililokua likirushwa na ITV kupitia Chemchem Art Group ya akina mzee Jengua, Tabia na wengineo.

Nakumbuka kipindi kile TV ipo moja kijiji kizima tu, saa 3 kamili usiku siku za jumatatu tunakusanyika kwenda kuangalia Kidedea. Kabla hujaanza kuwaangalia akina Jengua unakaribishwa na "Soundtrack" ya Jimmy Chocolate ambapo ndani yake kulikua na rap ya "Kidedea" Nakumbuka mpambano mkali wa mwaka 2001 pale Tripple A club ambapo mafahali watatu walipambanishwa pamoja. Ndanda Kossovo, Mao Santiago na Allan Mulumba Kashama.
Mimi nilikua natoa nafasi zaidi kwa Ndanda Kossovo au Allan Mulumba kutokana na nyinbo zake kali kama "Dar kibindankoi" iliyokuwa na rap maarufu kama "jumamosi jumamosi tulale wapi eeeh..".. na ile nyingine ya "oooh tupande kilimanjaro shuka mt.meru"..
Hata hivyo, Ndanda hakudumu sana na bendi hiyo baadaye alitimkia Marekani kwa shughuli za kimuziki, aliporejea Bongo alijikita mkoani Arusha na kuanzisha Kundi la Watoto wa Tembo kabla ya kuachana na bendi na vikundi na kuwa msanii anayejitegemea.
Kabla ya kukutwa na umauti, historia ya ugonjwa wake inaonesha alianza kusumbuliwa mwaka jana na tatizo la kupasuka kwa mmoja ya mishipa tumboni hivyo kutapika damu lakini madaktari walijitahidi akapona na kuendelea na shughuli zake. Ndanda alianza kuugua tena hivi karibuni akisumbuliwa na tumbo ambapo alilazwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar, mauti yalipomkuta majira ya asubuhi jana asubuhi.
Baadhi ya mafanikio aliyoyapata kwenye kazi yake ya muziki ni pamoja na kukubalika na kufahamika na watu wengi nchini, kumudu kuendesha maisha yake mwenyewe pamoja na familia.
Daaah all in all tumepoteza "icon" katika muziki wa dansi Tanzania. Ulale pema peponi Ndanda Kossovo "Kichaa".. Fikisha salamu zetu kwa kina Gabby Katanga, Abou Semhando a.k.a "Baba Diana", Banza Stone, Yusuph Chuchu a.k.a "Bwana Chuchu", Amina Ngaluma a.k.a "mwana Mahenge" na wakali wengine wa Dansi waliotangulia mbele za haki. Waambie tunawamiss sn.!


Imeandaliwa na Malisa GJ
Post a Comment
Powered by Blogger.