RAIS MAGUFULI AMTEUA MATHIAS CHIKAWE KUWA BALOZI JAPAN

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe. Picha ya Mtandaoni 

Rais John Magufuli amemteua Mathias Chikawe kuwa balozi wa Tanzania nchini Japan.
Taarifa iliyotolewa leo 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Chikawe umeanza Aprili 13, 2016.
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo Februari 15, 2016.
Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment
Powered by Blogger.