TIMU YA TAIFA YA ZIMBABWE KUWASILI LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya Zimbabwe inatarajiwa kuwasili leo Alhamisi mchana wakiwa na msafara wa watu 29, wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Zimbabwe ambao watafikia hoteli ya De Mag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.
Waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili leo mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili leo jioni kwa KQ.
Tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.
TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
Post a Comment
Powered by Blogger.