TANESCO YAMTIA MBARONI KINARA WA WIZI WA UMEME

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Polisi mkoani hapa, wamefanikiwa kumtia mbaroni mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa kinara wa wizi wa umeme anayedaiwa kuziunganishia nishati hiyo nyumba 30 kwa kupitisha nyaya chini ya ardhi.
Ofisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Mwanza, John Chilale amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya Tanesco kupokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa amewaunganishia umeme wakazi wengi wa maeneo ya Kitangiri, jijini hapa. Amedai kuwa mtuhumiwa alikuwa akiwatoza fedha watu wote aliowaunganishia umeme kulingana na vifaa vya umeme walivyo navyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangili, Said Lukonge amesema wizi huo ni hatari kwa maisha ya watu, kwani jinsi alivyoziungaisha waya, zinaweza kusababisha hitilafu muda wowote.
Mkazi mmoja wa eneo hilo, Joseph Kalula ni mmoja wa waliounganishiwa umeme kinyemelea, amesema alikuwa akitozwa Sh5,000 kila mwezi kama gharama ya umeme.
Mwananchi mwingine, Nadhilu Issa amesema alihamasika kuomba kuunganishiwa umeme na mtuhumiwa baada ya kuona majirani zake wakitumia umeme waliomweleza kuwa ni wa bei nafuu ikilinganishwa na ule wa Tanesco.
Kamanda wa
Post a Comment
Powered by Blogger.