PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA KUMI NA TISA(19)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.Ilipoishia. Shemeji aliniwekea Cd inayoonesha nikimlazimisha kufanya mapenzi (Nilimbaka) ENDELEA.
Nilijikuta nikishikwa na kizunguzungu pale pale na kuanguka chini. Nilikuja kushtuka nikiwa nimetundikiwa dripu ya maji nikiwa Hospital moja iliyokuwa pale mtaani kwetu. " Unajisikiaje shem?"aliniuliza baada ya kuona ninahangaika kuangalia mazingira yale " Niko sawa ila nini kimetokea? Na nimefika vip hapa?" nikauliza " Aaah! 
Ulipatwa na mshtuko kidogo na kupoteza faham ndo nikakuleta hapa" akajibu Nilitulia na kujalibu kuvuta kumbukumbu zangu na kufanikiwa kukumbuka kilichotokea na taratibu machozi yakanitoka. Shemeji alijitahdi kunibembeleza na kuniweka sawa mpaka nikawa vizuri tu Kwa sababu sikuwa na tatizo lolote lile baada ya ile dripu ya maji kuisha nilipewa ruhusa ya kurudi nyumbani. Shemeji alinifikishia chumbani kwake badala ya chu,bani kwangu. " S
amahani sana shemeji kwa kilichotokea,nimekaa na kutafakari nimegundua makosa yangu na nikwambie tu kuwa nimejilekebisha,nimeahirisha ule mpango" akasema Nilifurahi sana baada ya kusikia vile ingawa sikuamin kama kweli Shemeji kaghairi Nikatengenezewa chakula na shemeji mwenyewe kisha akanilisha na pia kuninunulia matunda yaliyosaidia kurudisha nguvu zangu. Kufikia asubuh afya yangu ilikuwa imetengamaa sana na nilijihisi ninanguvu za kutosha. 
Siku hiyo asubuh kaka alipiga simu tukaongea naye wote kwa pamoja kwa furaha na upendo Kaka alituambia kuwa atarudi baada ya siku tatu na kwa jinsi nilivyokuwa na ham naye nikataman awahi tu. Tulienda kazini kama kawaida na shemeji na kusimamia biashara vizuri na kitu nilichoshangaa ni shemeji kutotaja mambo yale tena wala mahusiano yetu. Jioni muda wa kurudi nyumbani Shemeji aliniaga kuwa ana udhuru kuna sehemu anaelekea kwanza atachelewa kuja kazini. 
Nilielekea nyumbani peke yangu bila shemeji na kuoga kisha nikakaa naangalia tamthilia ya Jumong peke yangu huku binti wa kazi akiwa jikon. Shemeji alirudi jioni ya saa moja na kumuondoa yule binti wa kazi jikoni na kisha akaingia yeye. Cha ajabu hata kile chakula alichopika yule binti Shemeji alikikataa na kunipikia kingine mwenyewe. Baada ya mapishi chakula kilitengwa kwenye sahani na kuletewa chumbani cha kwangu. 
Shemeji alikataa kula na mimi siku hiyo kwa kudai kuwa huko kwa rafiki yake alikopitia amekula na kushiba Alinilisha kile chakula taratibu mpaka kikasiaha. Baada ya kumaliza kile chakula nilianza kuhisi mabadiliko mengi kwenye mwili wangu. Kwanza nilijisikia mwepesi na mchangamfu sana utafikili nimekunywa pombe. Kisha nilisisimkwa sana mwilini na kutamani kufanya mapenzi,na nilikuwa namwangalia Shemeji kwa jicho la matamanio. 
Pale pale Shemeji alichukua simu na kumpigia kaka kisha wakaanza kuongea kimahaba Nilipatwa na wivu mkubwa sana mpaka nikabaki najishangaa Machozi yalikuwa yananitoka huku shemeji akiniangalia kwa makini. Alipokata simu nilimzaba kibao mpaka akaanguka chini " Unawezaje kuongea na huyo mbwa mbele yangu? Huniheshim? Nakuuliza huniheshimu? Basi huyo mbwa wako akirudi tu namuua tena kwa mkono wangu na wewe ukileta mdomo nakufyeka" niliongea bila kujitambua. Kumbe kile chakula kilifanya kazi kiliyokusudiwa kuifanya. 

ITAENDELEA JUMATANO
Post a Comment
Powered by Blogger.