PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Nilishtuka kusikia shemeji akisema vile,nikajua kuna kitu anamaanisha " Una maanisha nini shem?" nikamuuliza " Jaman! Ushapaniki tena? Sina maana mbaya wewe niambie tu" akajibu " Swala la kurithi huwa sio lazima ila huwa linatolewa kama shemeji atahitaj msaidizi atapewa ila halazimishwi" nikamjibu " Kwani shem nikuulize hunipend jaman?"akauliza "
 Yaani shem kwa mambo unayonipa nitakuwa mjinga sana kusema sikupendi" nikajibu " Sasa nisikilize,mimi nataka tuoane kwa namna yeyote ile sitaki hizi raha nizikose,akili kichwani,naomba usiniongeleshe mpaka utakapokubaliana na ombi lang" akasema Tulitoka tukiwa kama mabubu pale ndani na kuingia kwenye gari kisha safari ya kuelekea kazini ikiansa saa tano hiyo " Sioni umuhimu wa kunichunia shem bana" nikamwambia " 
Kama uko tayali niambie tuendelee kuongea"akajibu " Ok nambie niko tayali" nikasema " Mimi nataka tuoane na kutengeneza familia" akasema " Lakin kumbuka wewe ni mke wa kaka,itakuwaje?" nikamuuliza " Kwa namna yeyote ile tukiamua itawezekana," akajibu " Ndo unipe mpango wako,lakin jamii itatuchukuliaje lihali wewe ni mke wa kaka?" nikamuuliza " Huo uke unatoka wap? Ningekuwa nimeshazaa naye hapo sana lakin utasa ule naupeleka wapi?" akajibu ila akawa ameongea kitu kipya na kigeni sana kwangu " 
Utasa? Sijakwelewa" nikamwambia " Kwani hamjui kuwa kaka yenu tasa?" akaongea kwa nyodo Ilibidi nipaki gari pembeni na jasho lilinitoka " Nieleze vizur nikuelewe basi" nikamwambia " Ni hivi tuna miaka mingap kwenye ndoa na kakako?" akauliza " Minne sasa" nikajibu " Hujiulizi kwa nini hakuna kutapika? Au japo kula limao?" akasema " Tafadhal shem nieleze nielewe,hiyo inaweza kuwa mipango yenu bana" nikamwambia " 

Ni hivi baada ya mwaka bila mimba tuligombana sana na kakako mwishowe tukaenda kupima na ikagunduliwa kuwa mbegu zake haziwezi kurutubisha zangu namaanisha hawezi kumzalisha mtu" akajibu shemeji Nilipigwa na butwaa na kubaki na mshangao mkubwa sana,niseme ukweli mpaka nikajikuta machozi yananitoka " Kaka yangu" niliongea kwa upole " Sasa unalia nini? Mimi nimetumia akili badala ya
 kwenda nje au kutafuta mtu baki nimekupa nafasi ndg ili uzao uishie hapa hapa" akasema shemeji " Shem hili swala ni gumu kidogo,nnipe nafasi nifikirie kumbuka yule ni kakangu jaman,dam moja na mimi" nikamjibu " Wewe hujielew,hii ni nafasi itumie vizur bwege wewe,acha kuendelea kubaki wa kienyeji,hapa tumuondoe ili tule raha" akasema " Una maana gani? Tumuue?" nikauliza " Ndo hivyo wewe unafikiri nini?" akasema " 
Siwezi kumuua kakangu kwani hatuwezi kuendelea hivi hivi bila kumuua?" nikauliza " Nikipata mimba utakubali kumwambia kakako kuwa ni ya kwako? Hapa hakuna mjadala ni kumuondoa" akasema " Siwezi kumuua kwni hatuwezi kwenda mbali na kumuacha na maisha yake?" nikasema " Sikia acha ushamba,akiondoka itakuwa rahisi kukukubali unirithi ila akiwepo itakuwa ngumu" akasema " Siwezi" nikajibu " Endesha gari twende,nafikili hunijui" akasema Nilijalibu kumbembeleza wap? Alikuwa na hasira sana.

ITAENDELEA  ALHAMISI
Post a Comment
Powered by Blogger.