MHE. POSSI AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA SHULE NA VITUO VYA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI MANYARA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi ( wa pili kutoka kulia) akiwa katika ziara ya kutembelea shule ya msingi Katesh “A” na “B” ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa wa Manyara Machi 2, 2016. Kulia kwake ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw.Petro Tahan.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiangalia kiatu cha ngozi kilichotengenezwa na kikundi cha watu wenye ulemavu cha Ambiansi katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Machi 2, 2016.
Mmoja wa wanakikundi cha watu wenye ulemavu cha Ambiansi Bw. Marco Gidamicha akimkabidhi zawadi ya kikoi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi wakati wa ziara yake katika kituo hicho Machi 2, 2016 mkoa wa Manyara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza mtoto asiyeona Paulo Marcel (wa darasa la tatu) wakati walipokuwa wakionesha kwa vitendo namna watoto hao wanavyoweza kusoma kwa alama maalum wanazofundishwa katika shule ya msingi Katash “A” Wilayani Hanang Mkoani Manyara, tarehe 2, Machi, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post a Comment
Powered by Blogger.