MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI FEBRUARI, 2016 WAPUNGUA KWA ASILIMIA 5.6

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mkurugenzi wa Takwimu za Sensa na Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Februari, 2016. Kulia ni Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja.
Wapiga picha wakiwa kazini.


Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei katika Februari mwaka huu umepungua  mpaka kufikia asilimia 5.6  kutoka asilimia 6.5 ya  mwezi Januari.

Akizungumza  katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mkurugezi wa Sensa za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema kasi ya upunguaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka huu kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisiyakula kwa kipindi kilichoishia  cha Februlia, 20 ikilinganishwa na bei za Februari mwaka 2015.


Alisema kuwa mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Februari mwaka huu umepungua kwa  asilimia 10.3, mafuta ya dezeli kwa asilimia 4.5  na matunda kwa asilimia 7.2.


Kwesigabo alisema pamoja na kupungua kwa  kasi  ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kuna baadhi ya bidhaa zinaonyesha  kuongezeka  katika hicho  ni pamoja na Sukari kwa asilimia 7.1, Mkaa asilimia 4.3, Mchele kwa asilimia 22.9 na viazi 16.3.Aidha alisema hali ya mfumuko wa bei katika nchi za jilani unaelekea kufanana na nchi za afrika  mashariki ambapo Kenya umepungua hadi asilimia 6.84 kutoka  asilimi7.78 mwaka huu, Uganda umeongezeka kwa asilimia 7.7 kutoka  asilimia  7.6 kwa mwezi  Januari mwaka huu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Post a Comment
Powered by Blogger.