LEO KATIKA HISTORIA: IDI AMIN DADA MTOTO WA MGANGA WA JADI ALIYEITAWALA UGANDA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Amin alizaliwa mwaka 1925. Alilelewa na mama pekee baada ya baba kuitelekeza familia. Mama yake alikuwa ni mpigaramli na mganga. Alikua katika maadili na misingi ya Kikristo kabla ya kubadili dini na kuwa Muislamu.
Licha ya elimu yake ya Dini ya Kiislamu, hakuna kumbukumbu zinazoonyesha alisoma mpaka ngazi ipi. Lakini mwaka 1946 alijiunga na jeshi la kikoloni, King’s African Rifle (KAR) lililokuwa chini ya Waingereza.


Aliingia kama mpishi. Baadaye alipanda vyeo kutokana na uhodari wake katika mambo mengi. Alipanda mpaka cheo cha juu kabisa ambacho Waafrika walikuwa wanaishia. Ikumbukwe kuwa KAR ilikuwa na askari wazungu pia.
Mwaka 1961 alipandishwa cheo na kuwa Luteni. Walikuwa Waafrika wawili pekee waliofanikiwa kupata cheo hicho. Yeye na Milton Obote, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu na kisha rais wa kwanza wa nchi hiyo.

Februari 2, 1971 Uganda ilipata Rais wa kwanza aliyeingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi. Huyo alikuwa ni Idi Amin Dada. Aliitawala nchi hiyo kwa miaka minane mfululizo mpaka alipoondolewa na majeshi ya Tanzania chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere.

Amin na Obote walikuwa maswahiba. Walifanya mambo mengi pamoja. Mwaka 1965 walipata kashfa ya kufanya magendo. Ilikuwa ni biashara ya pembe za ndovu na dhahabu kutoka Zaire. Ilikuwa ni kazi ya wawili hao na waasi walioipinga Serikali ya Patrice Lumumba.


Mwaka mmoja baadaye Bunge lilitaka uchunguzi wa kashfa hiyo. Mara moja Obote alibadili katiba ya nchi hiyo na kujipandisha cheo na kuwa rais. Alimpandisha cheo Amin pia ambaye alikuwa kanali aliyeongoza kikosi cha anga.
Amin alipanda vyeo mpaka kuwa mkuu wa majeshi wa nchi hiyo. Lakini mwaka 1970 rais alimpunguzia madaraka na kumfanya mkuu wa Jeshi la Ulinzi pekee. Hiyo ilitokana na taarifa za matumizi mabaya ya fedha na Rais alikuwa amepanga kumkamata. Habari hizo zilimfikia Amin ambaye naye alipanga mapinduzi ya kijeshi.


Januari 25, mwaka 1971, Amin alitekeleza mapinduzi hayo. Alifanya hivyo wakati Obote akiwa ameenda Singapore kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola. Wiki moja baadaye alijitangaza kuwa rais wa taifa hilo. Muda mfupi baada ya kuingia Ikulu aliwaachia wafungwa wa kisiasa na kuahidi kuitisha uchaguzi huru.


Aliwahi kukaririwa akisema kuwa lengo lake ni kuondoa ufisadi serikalini na utumwa. Aliahidi kuwa baada ya kuondoa madhila hayo basi uchaguzi wa kidemokrasia ungefanyika. Hilo halikufanyika. Mwaka 1972 aliwaondoa wafanyabiashara wote wenye asili ya Asia na miradi waliyokuwa nayo akaikabidhi kwa waliomuunga. Aliwaua wote walioonekana kumpinga. Wengi walikimbia na kuishi uhamishoni. Mawaziri wake pia walifanya hivyo.


Miongoni mwa makosa aliyoyafanya ni kutangaza vita dhidi ya Tanzania. Hiyo ilikuwa ni baada ya makamu wake, Jenerali Mustafa Adrisi ambaye alinusurika katika ajali ya gari iliyotokea Novemba 1978. Hiyo ilisababisha baadhi ya askari wake kuasi na kukimbilia Tanzania.
Kutokana na hilo Amin aliamini kuwa Serikali ya Tanzania ilikuwa inamhujumu hivyo aliamua kuishambulia kijeshi. Baada ya mapigano ya miezi minne mfululizo, alishindwa vita na akalazimika kukimbia.


Hakupata bahati ya kurudi tena katika ardhi ya nchi yake mpaka mauti yalipomkuta. Amin alifariki akiwa uhamishoni huko Saudi Arabia, Agosti 16, 2003.
Post a Comment
Powered by Blogger.