LEO KATIKA HISTORIA: HUYU NDO EDWARD MORINGE SOKOINE SHUJAA WA WANYONGEMZALENDO WA TANGANYIKA, ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Hayati Sokoine alizaliwa mnamo mwaka 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND ambayo kwa sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli, wilaya iliyoko mkoani Arusha. Hayati Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli, akafaulu kujiunga na shule ya sekondari Umbwe, hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958, alipomaliza hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961, kisha alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963 kusomea mambo ya uongozi na utawala na aliporudi akateuliwa kuwa afisa mtendaji wilaya ya Maasai Land, na kutokana na utendaji wake uliotukuka wilayani Monduli wananchi hawakuwa na budi kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge wa Monduli na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa serikali na hayati baba wa taifa Nyerere na akachaguliwa kuwa Naibu wa wizara ya mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967, kama hiyo haitoshi nyota ya kiuongozi ilizidi kumwangazia ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa waziri wa Usalama na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa waziri mukuu wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika,na Muungano wa Tanzania.

Hayati sokoine alikuwa hasa mzalendo na aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusisimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje, hii ilikuwa mwaka 1981 mpaka 1983 alirudi kuendelea kama waziri mkuu kuanzia wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube, eneo la Wami Dakawa sasa Wami Sokoine mkoani Mororgoro, ajali iliyopelekea mauti yake palepale, kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi na kwa bahati mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika kusini anakula bata.


"Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali,kuiba,kuhujumu uchumi,kupokea rushwa,maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"

Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine, wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984, takribani miaka 30 iliyopita,wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini,ulangunguzi,rushwa na biashara ya magendo,enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto,lakini mpaka leo kauli yake inaishi,inatumika,inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili,misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali, leo tunamkumbuka, tunakumbuka kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake, lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je? utakapofariki utakumbukwa kwa lipi? je viongozi wetu wanaishi kimatendo kma hayati wetu Sokoine?


UTATA WA KIFO CHAKE NA MASWALI MAGUMU YASIYOJIBIKA KIRAHISI

Itakumbukwa kwamba karibia viongozi wakubwa wote wa serikali waliondoka mjini Dodoma kwa ndege mara baada ya kikao cha NEC, Isipokuwa hayati Sokoine, yeye alisema wazi ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,hivyo alipendekeza kusafiri kwa njia ya barabara ili ajionee Mashamba makubwa na maendeleo ya kilimo kwa ujumla,

Gari lililomgonga liliwezaje kupenya magari yote yaliyokuwa kwenye msafara wa waziri mkuu Sokoine mpaka kulifikia gari la marehemu Sokoine na kuligonga?vp trafiki walikuwa wapi mpaka lori hilo limfikie kiongozi huyo?vipi maafisa wa ulinzi ambao kazi yao ni kumlinda?


Katika ajali hiyo aliyefariki ni hayati Sokoine pekee,vpi kuhusu wengine kwani hakuna hata aliyejeruhiwa pakubwa


Aliyesababisha ajali hiyo alikuja kuachiwa huru na akarudishwa kwao Afrika kusini,


TETESI JUU YA UTATA WA KIFO CHAKE

Ni ukweli kwamba ukiwa kiongozi unaetimiza majukumu yako kikamilifu ni lazima utakuwa na maadui wengi na wanaokutafta kwa kila namna,hayati sokoine kutokana na vita yake dhidi ya Wahujumu uchumi,mtakumbuka wakati wa vita hiyo kuna watu walienda kuficha bidhaa mapolini na wengine kumwaga mitoni,baharini na ziwani,hali ilikuwa tete kwa wahujumu uchumi pia Walanguzi,wazee wa Magendo,wala rushwa na watendaji wazembe wa serikilini,na hapa anatajwa mzee Kawawa kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliokemewa na maremu wakati wa kikao hicho cha mwisho mjini Dodoma,
Pia inadaiwa aliiva katika misingi ya kijamaa kupita kiasi,hali ambayo ilimtisha hata baba wa taifa
Je ni ajali ya kawaida iliyotokana na mikono na mapenzi ya Mungu?ama mkono wa binadamu?swali hili ni gumu na lina dead end

MCHANGO WAKE KWA TAIFA NA MISIMAMO NA MITAZAMO YAKE

1:Aliamini katika Haki, Usawa na uwajibikaji
2:Aliamini katika siasa za ujamaa zaidi ya siasa yeyote ile.
3:Aliamini kwamba maendeleo huja kwa watu kujituma kufanya kazi halali na bidii.
4:Aliamini katika mabadiliko chanya
5:Alikuwa mzalendo hasa kwa taifa hili
6:Aliichukia vitendo vya rushwa, hujuma, uhujumu uchumi, ulanguzi na magendo.
7:Alikuwa mtu wa vitendo na kamwe alikuwa si mtu wa kupenda kulalamikalalamika.

MCHANGO WAKE KITAIFA


1:Alikuwa mstari wa mbele enzi za vita ya Kagera pindi tunampiga Nduli Idd Amini.

2:Alianzisha vita dhidi ya uhujumu uchumi, biashara ya Ulanguzi, Magendo na aliichukia Rushwa kwa vitendo
3:Alikuwa mzalendo wa kweli wa taifa hili.
4:Aliamni katika siasa na kilimo,akiamini kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hii ilipelekea kutotaka kupanda ndege ili ashuhudie juhudi kubwa za Watanganyika katika suala la kilimo
5:Alitunza na kutukuza tamaduni za kiafrika na utaifa wa mtanzania.

Hitimisho, leo ikiwa imepita takribani miaka 30,tangu shujaa wetu na mzalendo hayati Edward Moringe Sokoine tangu atangulie mbele ya haki, je viongozi wetu wa sasa wanaishi na kutenda kwa ajili ya manufaa ya umma kama hayati Sokoine? je? Pengo lake limezibika ama bado?wito wangu kwa wanasiasa wetu nchini wasilitumie jina la kiongozi wetu huyu na baba wa taifa kwa ajili ya kunufaika kisiasa tu?wakati hawamaanishi kwani kuchagua uovu kwenye njia ya haki ni dhambi,na sikuzote ukiwa safarini huwaulizi njia wasafiri wenzako bali wale watokao huko.


Mungu aipe pumziko la amani nafsi yake na amlaze pema peponi hayati Sokoine 


Imeandaliwa na  Nicholaus Kilunga
kilunganicholaus@yahoo.com
Kibondo, Kigoma, Tanzania
Post a Comment
Powered by Blogger.