JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LIMEFANYA MSAKO NA KUKAMATA SILAHA 26 AINA YA GOBORE NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA MAGOBORE HAYO.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msadizi wa Polisi Lazaro Mambosasa – ACP akionyesha mitambo ya kutengenezea Magobore hayo baada ya kufanya msako mkali katika Wilaya zake zote na kukamata makosa mbalimbali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa akionyesha Magobore yaliyokamatwa katika msako mkali katika Wilaya zake zote na kukamata makosa mbalimbali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.

RPC Dodoma Lazaro Mambosasa - ACP akionyesha golori zinazotumika katika magobore hayo baada ya kumalizika kwa Operesheni na Msako mkali katika Wilaya zake zote na kukamata makosa mbalimbali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanya Operesheni na msako mkali katika Wilaya zake zote na kukamata makosa mbalimbali. Operesheni hiyo ilianza kufanyika tarehe 22/02/2016 hadi 06/03/2016.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msadizi wa Polisi LAZARO MAMBOSASA – ACP amesema katika Operesheni hiyo jumla ya silaha haramu 19 aina ya Gobore zimesalimishwa na silaha saba (7) zimekamatwa za watu waliokaidi utii wa sheria, mitambo miwili ya kutengeneze silaha hizo haramu imekamatwa pamoja na watuhumiwa saba.
Kamanda MAMBOSASA amesema watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha MANDA Tarafa ya MPWAYUNGU Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma  na wamekuwa wakimiliki silaha hizo kinyume cha sheria  na wakizitumia katika uhalifu mbalimbali hasa uwindaji haramu katika hifadhi ya RUAHA inayopakana na mkoa wa Iringa.
Aidha Kamanda MAMBOSASA amesema kutokana na operesheni hiyo watu 19 waliweza kusalimisha silaha zao katika ofisi za serikali za vijiji na hawakuchukuliwa hatua kwa kuwa walitii sheria bila shuruti.
Vilevile Kamanda MAMBOSASA amesema katika Wilaya za Dodoma, Kondoa na Kongwa walikamatwa watuhumiwa 32 wa makosa ya Kupatikana na Bhangi, jumla ya misokoto misokoto 672 ilikamatwa.  Watuhumiwa 11 walikamatwa kwa kosa la Kupatina na Pombe haramu ya Moshi na jumla ya lita 260 zilikamatwa.  Watuhumiwa 7 walikamatwa kwa kosa la Kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Mirungi Kilogram 43.
Pia Operesheni ilihusisha makosa ya Usalama barabarani na kukamatwa kwa jumla ya pikipiki 265 kwa makosa mbalimbali, ambapo pikipiki 241 zilitozwa faini na kiasi cha fedha Tsh. 7,230,000/= zilipatikana kutokana na tozo. 
Kamanda MAMBOSASA ametoa wito kuwa msako mkali unaendelea na watu wote wanaomiliki silaha haramu kinyume cha Sheria wasalimishe silaha hizo kwa hiari kwenye  Ofisi za Serikali na vituo vya Polisi mapema iwezekanavyo na hawatachukuliwa hatua.  Wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha Sheria wasiotayari kusalimisha wafichuliwe ili wachukuliwe hatua za kisheria dhidi ya umiliki haramu wa silaha. Aidha wananchi waache kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa aina yoyote na kufanya kazi halali kujipatia kipato halali kwa familia zao kwani msako utakuwa endelevu wasije wakaishia jela na kuziacha familia zao zikiteseka.
Katika matukio mengine Kamanda MAMBOSASA amesema mnamo tarehe 07.03.2016 majira ya saa 16:00 huko katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la BASILI MSABILA mwenye miaka 24, Mwanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa - HOMBOLO Dodoma ngazi ya cheti, alifariki dunia wakati anatibiwa baada ya kujeruhiwa kichwani kwa chuma na Mwanafunzi mwenzake aitwaye CHARLES MAKELE, miaka 19, mwenye miaka 19 mwanafunzi ngazi ya cheti kozi ya utawala chuo cha TAMISEMI Hombolo.  
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania chaja ya simu mali ya marehemu, katika chumba cha bweni lao wanaishi wanafunzi wanne ambapo siku ya tarehe 6/03/2016 hakukuwa na umeme na uliporudi umeme wanafunzi hao walianza kugombani chaja hiyo ya simu ugomvi uliopelekea kuanza kupigana na  ndipo BASILI MSABILA kujeruhiwa kwa chuma chenye ncha kali kichwani na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na kufariki dunia akiwa kwenye matibabu siku iliyofuata. Mtuhumiwa amekamatwa na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unendelea.
Vilevile Kamanda MAMBOSASA amesema tukio lingine limetokea tarehe 07.03.2016 majira ya saa 21:00hrs huko eneo la Kisasa Manispaa ya Dodoma ambapo mtu mmoja mwanaume asiyefahamika jina mwenye umri kati ya miaka 23-25 aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mtu/watu waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kujaribu kuvunja dirisha la nyumba akiwa na wenzake waliofanikiwa kukimbia. Uchunguzi unaendelea na Juhudi za kuwatafuta watu waliohusika na mauaji hayo zinafanyika. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma LAZARO MAMBOSASA – ACP ametoawito kwa wananchi wa Dodoma kutojichukulia sheria mkononi na kutofanya mauaji ya kikatili dhidi ya watu kwa tuhuma nyepesi kwa kisingizio cha watu wenye hasira kali. Vitendo hivi havitavumilika na sheria zifuatwe kila mtu ana haki ya kuishi na kujitetea mbele ya sheria.

Post a Comment
Powered by Blogger.