DKT. SHEIN AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MZEE HAMID AMEIR MUASISI WA MAPINDUZI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakibeba jeneza la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuswaliwa leo wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Wananchi waliohudhuria katika mazishi ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM wakilibeba jeneza wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na wananchi na Viongozi wakiwa katika maziko ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM aliyezikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kufariki jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuzikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua iliyoombwa baada ya kuzikwa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akisoma risala ya na wasifu wa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuzikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.Picha na Ikulu.
Post a Comment
Powered by Blogger.