WAZIRI KITWANGA AKABIDHIWA RIPOTI YA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA KUBORESHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akipokea ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akisaini ripoti aliyokabidhiwa na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia), kwa ajili ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Issa alisema Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) na Maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kukabidhiwa ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Katika hotuba yake, aliwataka Polisi wahakikishe wanautekeleza Mpango huo na kila wiki ameagiza apewe ripoti ya utekelezaji huo unaotarajiwa kuanza katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni na baada ya hapo utasambaa nchi nzima. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu. Kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi lake. Waziri Kitwanga alikabidhiwa ripoti hiyo na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia) katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na baada ya hapo utasambaa nchi nzima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment
Powered by Blogger.