SERIKALI YAPELEKA TANI 200 ZA MAHINDI YA CHAKULA CHA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akieleza maamuzi ya serikali kupeleka chakula cha msaada kwa Waathirika wa maafa ya mafuriko wa kijiji cha Ikwiriri wilayani Rufiji, tarehe 16 Februari, 2016.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akifafanua masuala ya menejimenti ya maafa ya mafuriko alipofika wilayani Rufiji kukagua athari za maafa hayo, (wa kwanza kushoto)  ni Mbunge wa jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti, Ally Ungwando na kulia kwake ni Mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu, tarehe 16 Februari, 2016.
 Mkazi wa kijiji cha Mayuyu wilayani Rufiji, Suleiman Idd akishukuru kwa serikali  kuwapatia chakula cha msaada waathirika wa  maafa ya mafuriko kijijini humo wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (hayupo pichani), alipofika kijijini humo kukagua athari za maafa hayo tarehe 16 Februari, 2016.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akiangalia sehemu ya njia iliyokuwa ikitumiwa na wananchi wa kijiji cha Utete wilayani Rufiji ambayo kwa sasa wanatumia mitumbwi kuvuka kuelekea kijijini humo kutokana na njia hiyo kufurika maji, wakati akikagua athari za maafa ya mafuriko wilayani humo ,  tarehe 16 Februari, 2016.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama  akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mayuyu wilayani Rufiji wakati alipofika kijijini humo kukagua athari za maafa ya mafuriko tarehe 16 Februari, 2016.
Post a Comment
Powered by Blogger.