“PENZI LA SHEMEJI” SEHEMU YA TATU(3)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Tulipofika nyumbani nilipitiliza chumbani kwangu na kuwaacha shemeji na kaka wakiwa wamekaa sebuleni wakiongea Nilibaki na mawazo sana juu ya lile ombi la shemeji kuwa nishare na kaka kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya " Lakin shemeji ni mzur!! Ila siku kaka akijua itakuwaje? Si ndo ataniua na ukiangalia kaka anavyonipenda!! 
Dah! Mungu nisaidie" nikaendelea kuwaza Nilipitiwa na usingizi bila kujielewa mpaka nilipokuja kushtuliwa na msaidizi wa kazi usiku " Kaka chakula tayali" alisema Uzuri wa kaka na alichowahi kunieleza na nilishapanga kukifanyia kazi ni kwenye swala la msaidizi wa kazi Kaka ana style moja nzur sana ya kuajili wafanyakazi wa ndani wamama watu wazima au mabinti wabaya sana kwa sura Anaamin hilo linampunguzia vishawishi na pili sisi vijana tunaopita pale kwake hatutaweza kufanya ujinga wowote nao. Na kweli ukimuangalia yule binti aliyekuwa pal naamin hautamwangalia tena Alikuwa na sura nzito sana,na ukikosea ukakutana naye asubuh hajanawa uso nahisi hata chakula utashindwa kula. Nilienda kula na wao mezani,nashukuru kiti anachokaa shemeji kilikuwa mbali na mimi hivyo asingeweza kufanya chochte Baaada ya kukaa nilimpiga jicho nikashangaa akinikonyeza Nikageuka mapema na kukaa nisije nikashtukiwa na kaka Tulianza kula taratibu huku nikiwa kimya nikiwasikiliza wao wakiongea Dogo vip?mbona leo umepooza wakati wewe ndo muongeaji sana?" aliuliza kaka " Sijisikii vizur kaka" nikasema " 

Angalia kama hali sio nzuri uende kuchek afya dogo" akasema " Usijal kaka nitakuwa poa tu" nikasema Tuliendelea kula huku waongeaji wakubwa wakiwa kaka na mkewe " Jamani wiki ijayo nitasafiri kwenda Dubai kufata mzigo" akasema kaka " Mbona ghafla?" nikajitia kuuliza utafikiri sijui " Mzigo umeisha dukani mdogo wangu hivyo napaswa kuufata" akasema " Ok,unaondoka lini?" nikauliza " Jumapili nitaondoka" akasema " Baby nitakumis sana,af nikwambie?" akasema shemeji " Usijal baby hata mimi nitakumic,nambie?" akasema kaka " Nimemic sana kuku wa kienyeji" akasema " 
Basi kesho nitakununulia uwakaange baby" akasema kaka " Hapana,usinunue,kwa saababu wewe unaenda huko,kuna vitu utakula huko ambavyo me sitavipata na mimi ukiondoka nitakula kuku wa kienyejo" akasema " Hahahahaha! Aya bana we mshindi" akasema kaka " Ila nataka uniruhusu ukiondoka nile kuku wa kienyeji" akasema Shemeji Nilishtukia yale maongezi kuwa yananihusu mimi ila kaka ndo hajaelewa kabisa " 
Me nashaur kaka usimruhusu mpaka urudi mule wote" nikachangia " Kwa nini mdogo wangu? Unajua kabisa ninavyompenda mke wangu,asina namna ya kumzuia dogo acha afaid na isitoshe na wewe upo utafaid au wewe hupend?" akaongea kaka bila kujielewa " Dah! Napenda kaka ila sidhani kama tutakutendea haki kula peke yetu" nikasema " Wee shem naye! Mmmh! Acha ushamba bana" akasema shemeji.

ITAENDELEA JUMATATU
Post a Comment
Powered by Blogger.